Star Tv

Serikali imepokea msaada wa Faranga za Uswisi Milioni 15.75 sawa na shilingi Bilioni 39.59 kwa ajili ya kugharamia mradi wa uboreshaji na uimarishaji wa mfumo wa afya pamoja na kugharamia program ya kutokomeza Malaria nchini.

Msaada huo umepokelewa na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Bwana Doto James ambaye amesema lengo kuu la msaada huo ni uanzishwaji wa huduma ya msaada wa kitaalamu kwa Serikali chini ya utaratibu wa kituo cha kuimarisha mifumo ya afya kilichopo Ofisi ya Rais TAMISEMI.

Bwana James alisema msaada huo utatumika kuwezesha mpango wa kudhibiti Malaria Tanzania ili kuondoa kabisa vifo vinavyotokana na malaria na kupanua wigo wa maeneo yasiyokuwa na malaria.

Bw. James alilifafanua  kuwa, hii ni mara ya pili katika kipindi cha siku 30 zilizopita kwa Serikali ya Uswisi kuipatia Tanzania msaada wa kuboresha masuala ya afya ambapo tarehe 6 Oktoba, 2020 nchi hiyo iliipatia Tanzania shilingi Bilioni 44.10.

Kwa upande wake Balozi wa Uswisi nchini, Mhe. Didier Chassot amesema tangu mwaka 2001, Uswisi kwa kushirikiana na Tanzania imekuwa ikitekeleza mapambano dhidi ya malaria kupitia program mbalimbali zenye lengo la kuisaidia nchi kufikia malengo iliyojiwekea kupitia Mpango wa Maendeleo wa Miaka Mitano.

Aidha, Katibu Mkuu Wizara ya afya, Jinsia, Wazee na Watoto, Mkurugenzi wa Kinga Wizara hiyo, Dkt. Leonard Subi, alisema msaada huo utasaidia kuendeleza mafanikio yaliyopatikana hasa upatikanaji wa dawa na kuimarisha mifumo ya takwimu katika sekta ya afya nchini.

Latest News

“MAISHA HAYAJI MARA MBILI, TUSIPOTOSHE KUHUSU CHANJO”-IGP. Simon Sirro.
29 Jul 2021 11:30 - Grace Melleor

Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP. Simon Sirro, amewataka Wananchi na Watanzania kwa ujumla wasidanganywe na watu wacha [ ... ]

“MIMI NI MAMA, BIBI, MKE NA RAIS, SIWEZI KUJIWEKA KATIKA HATARI”-Rais Samia....
28 Jul 2021 10:26 - Grace Melleor

Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amepokea chanjo dhidi ya Ugonjwa wa COVID-19, Ambayo ameizindua leo Julai 28, Katik [ ... ]

MSICHANA AUAWA KWA KUVAA JEANS.
28 Jul 2021 09:51 - Grace Melleor

Msichana mmoja aliyejulikana kwa jina la Neha Paswan, mwenye umri wa miaka 17, anadaiwa kupigwa hadi kufa na watu wa fam [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2021 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.