Star Tv

Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) imefafanua kuhusu taarifa zinazosambaa mitandaoni kuhusiana na utaratibu wa kupata majibu ya maombi ya mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu katika mwaka wa masomo 2020/2021.

Taarifa iliyotolewa leo Oktob 19, na Mkurugenzi Mtendaji wa HESLB, Abdul-Razaq Badru amesema HESLB bado haijatoa orodha ya wanafunzi waliopangiwa mkopo na kuwa kwa sasa, kazi ya uchambuzi wa maombi ya mkopo yaliyowasilishwa inaendelea.

Badru amesema taarifa hizo zisizo sahihi zinazosambaa mitandaoni zinawaelekeza waombaji mikopo kupakua mfumo (application) katika simu zao utakaowawezesha kuona orodha ya wanafunzi waliopangiwa mkopo kwa mwaka 2020/2021.

“Taarifa rasmi kuhusu HESLB, zikiwemo zinazohusu wanafunzi wanaopangiwa mkopo zitatolewa kuanzia Novemba 10, 2020 kupitia akaunti walizotumia kuomba mkopo inayofahamika kama SIPA – Student’s Individual Permanent Account,’’ amesema Badru.

Badru ameongeza kuwa taarifa kuhusu wanafunzi waliopangiwa mikopo pia zitatolewa kupitia vyombo vya habari, tovuti ya HESLB na mitandao ya kijamii ya HESLB.

Serikali imetenga kiasi cha Tsh Bilioni 464 katika mwaka wa masomo 2020/2021, zinazotarajia kusomesha jumla ya wanafunzi 145,000 wakiwemo wanafunzi 54,000 wa mwaka wa kwanza na wanafunzi 91,000 wanaoendelea na masomo katika taasisi mbalimbali za elimu ya juu nchini.

Latest News

Mgogoro wa Maji unatishia Amani Duniani, inasema ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa...
21 Mar 2024 14:18 - Kisali Shombe

Siku ya Maji Duniani ambayo inafanyika tarehe 22 Machi ikiwa na kaulimbiu: 'Maji kwa Ustawi na Amani. Ambapo maji ni moj [ ... ]

Matarajio katika mkutano wa BRICS nchini Afrika Kusini, Jumanne tarehe 22/2023
21 Aug 2023 12:14 - Kisali Shombe

Mkutano huo ambao utafanyikia Johannesburg nchini Afrika Kusini siku ya Jumanne, tarehe 22 Agosti 2023, unatarajiwa kuhu [ ... ]

Rais Ramaphosa Kuwa Mwenyeji wa Rais Xi Jinping wa China
21 Aug 2023 11:11 - Kisali Shombe

Rais Cyril Ramaphosa Jumanne ya tarehe 22 Agosti 2023, atakuwa mwenyeji wa Mheshimiwa Rais Xi Jinping wa China katika Zi [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2024 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.