Star Tv

Tume ya uchaguzi nchini Tanzania (NEC) imepinga taarifa zilizotolewa kwenye vyombo vya habari na mitandao ya kijamii na Katibu mkuu wa chama cha upinzani nchini humo Chadema, Bw John Mnyika.

Tume imepinga taarifa iliyotolewa na Bwana Mnyika kuhusu mchakato wa zabuni ya uchapishaji wa makaratasi ya kupigia kura pamoja na jina la mzabuni.

Tume hiyo imezitaja taarifa za CHADEMA kuwa ni za upotoshaji, na kuongeza kuwa manunuzi ya jumla ya zabuni 47 ziliorodheshwa ikiwemo zabuni iliyoyohusu uchapishaji wa karatasi za kupigia kura na njia ya kumpata mshindi iliyotangazwa ni ya ushindani wa wazi wa kimataifa.

Taarifa hiyo ya NEC imetolewa baada ya Chama cha Chadema kupitia Katibu wake Mkuu Bw John Mnyika kuitaka NEC kutaja kampuni ya uchapishaji wa karatasi za kupigia kura. Bwana Mnyika amesema hayo katika mazungumzo na waandishi wa habari:

’’Kuna jambo ambalo naamini waandishi wa habari hamlifahamu na umma haulifahamu na kupitia kwenu ni vizuri jambo hili likawa wazi kwa umma, tarehe nane mwezi Oktoba, Tume ya uchaguzi iliitisha kikao cha kwanza cha tume ya taifa cha manunuzi na lojistiki... tafsiri yake ni nini?...toka mchakato wa uchaguzi umeanza, tume ya taifa ya uchaguzi imekuwa ikifanya manunuzi na kufanya lojistiki mbali mbali za uchaguzi bila kuhusisha vyama vya siasa mpaka tarehe nane Oktoba, wameita kikao ambacho kimsingi ni kuvieleza tu vyama kwamba tayari tume imekwisihafanya manunuzi ya vifaa vya kiuchaguzi katika masuala ambayo yanapaswa kuwa wazi kwa umma’’-Mnyika amesema.

Taarifa hiyo iliyotolewa na Mkutugenzi wa uchaguzi NEC Dkt. Wilson M.Charles imesema licha ya Tume kuvishirikisha vyama vya kisiasa kwenye eneo la upatikanaji wa vifaa vya uchaguzi kikiwemo Chadema vyama hivyo havikuteua wajumbe wa kuunda kamati ya Lojistiki, licha ya vyama hivyo kuandikiwa barua na tume tarehe 30 Juni, 2020.

Tume ya uchaguzi nchini ndio yenye mamlaka ya kikatiba ya kusimamia na kuratibu uendeshaji wa uchaguzi wa Rais Wabunge na Madiwani kwa upande wa Tanzania bara.

Latest News

WATANZANIA WATAKIWA KUENDELEA KULIPA KODI BILA KUCHOKA.
14 Jun 2021 19:01 - Grace Melleor

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amewataka watanzania kuendelea kujitoa kulipa kodi ili kuwez [ ... ]

WAZIRI MKUU MPYA AAPA KUIUNGANISHA ISRAEL.
14 Jun 2021 06:33 - Grace Melleor

Waziri Mkuu mpya wa Israel Naftali Bennett ameapa kuliunganisha taifa hilo ambalo linalezwa kufadhaishwa na chaguzi nne  [ ... ]

RAIS SAMIA AZINDUA KIWANDA CHA KUSAFISHA DHAHABU NA JENGO LA BOT.
13 Jun 2021 14:11 - Grace Melleor

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amezindua kiwanda cha kusafisha dhahabu jijini Mwanza kinach [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2021 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.