Star Tv

Mwanamume mmoja ambaye ana umri wa miaka zaidi ya 80 nchini Ufaransa, ameilipua sehemu ya nyumba yake wakati alipokuwa akijaribu kumuua nzi.

Imeelezezwa kuwa mwanamume huyo alikuwa anakaribia kula chakula chake cha jioni na alikasirishwa na kelele ya nzi aliyekuwa anamzunguka.

Mwanamume huyo aliamua kuchukua kifaa cha umeme kilichotengenezwa kwa ajili ya kuwaua mende akaanza kumuua nzi huyo lakini kwa bahati mbaya gesi ilikuwa inavuja katika nyumba iliyopo kando ya mto Dordogne nchini Ufaransa.

Aidha, gesi na kifaa chake vilisababisha mlipuko na sehemu ya paa la nyumba yake iliyopo katika kijiji cha Parcoul-Chenaud kuharibika.

Kulingana na taarifa za vyombo vya habari nchini humo, mwanaume huyo ambaye hakuwa na silaha alibahatika kutoroka akiwa ameungua tu kwenye mkono wake.

Hata hivyo hatma ya nzi huyo aliyekuwa akimsumbua bado haijajulikana chombo cha habari cha Sud-quest kilisema.

Mwanaume huyo kwa sasa amejihifadhi katika hoteli moja ya eneo hilo huku familia yake ikikarabati nyumba yake.

Mwisho.

Credits: BBC Swahili.

Latest News

ETHIOPIA YASEMA HAITISHWI NA TAMKO LA RAIS DONALD TRUMP.
24 Oct 2020 16:54 - Grace Melleor

Waziri mkuu wa Ethiopia amesema nchi yake "haitakubali vitisho vya aina yoyote" baada ya Rais Donald Trump kusema kuwa M [ ... ]

RAIS TSHISEKEDI ATANGAZA MASHAURIANO YA UMOJA KWA MUUNGANO TAWALA.
24 Oct 2020 06:41 - Grace Melleor

Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Felix Tshisekedi, katika hotuba yake kwa taifa aliyoitoa siku ya Ijumaa wiki hi [ ... ]

SEKTA YA AFYA NCHINI YAPATA NEEMA KUTOKA USWISI.
23 Oct 2020 15:23 - Grace Melleor

Serikali imepokea msaada wa Faranga za Uswisi Milioni 15.75 sawa na shilingi Bilioni 39.59 kwa ajili ya kugharamia mradi [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2020 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.