Star Tv

Wafanyakazi wa uokoaji nchini Lebanon wanasaka zaidi ya watu 100 waliotoweka kufuatia mlipuko mkubwa uliokumba eneo la bandari ya mji mkuu wa Beirut siku ya Jumanne.

Mlipuko huo ambao umewaua takribani watu 100 kufikia sasa na kuwajeruhi wengine 4,000, umefanya mji wote kuyumbishwa na mlipuko huo ulioanza kwa moto katika bandari kuliko sababisha kutokea kwa wingu kama la uyoga.

Raisi Michel Aoun alisema kwamba tani 2,750 za ammonium nitrate zilikuwa zimewekwa vibaya katika ghala moja kwa miaka sita.

Rais Aoun ameitisha kikao cha dharura siku ya leo Jumatano na kutangaza hali ya dharura ya wiki mbili, pia ametangaza kwamba serikali itatoa dola milioni 66 za hazina ya dharura. ''Kile tunachoshuhudia ni janga kubwa'', alisema mkuu wa kundi la msalaba mwekundu George Kettani akizungumza na vyombo vya habari. ''Kuna waathiriwa kila mahali''.

Aidha, Maafisa walisema siku ya Jumanne kwamba uchunguzi unaendelea ili kubaini chanzo kilichosababisha mlipuko huo huku Baraza kuu la ulinzi nchini Lebanon lilisema kuwa wale waliohusika wataadhibiwa vilivyo.

Mlipuko huo umejiri wakati mgumu kwa upande wa taifa hilo huku likikabiliwa na mgogoro wa kiuchumi unaosababishwa na mgawanyiko wa jadi pamoja na mgogoro mwingine wa virusi vya corona.

Hali ya wasiwasi pia ilikuwa juu kabla ya uamuzi wa siku ya Ijumaa kuhusu kesi ya mauaji ya aliyekuwa waziri mkuu Rafik Hariri 2005.

Latest News

JAJI MKUU WA KENYA AMSIHI RAIS KENYATTA KULIVUNJA BUNGE.
22 Sep 2020 10:22 - Grace Melleor

Jaji Mkuu wa Kenya David Maraga, amemshauri rais wa nchi hiyo Uhuru Kenyatta, kulivunja bunge la kitaifa na lile la Sene [ ... ]

“IRAN ITAJIBU VIKALI UONEVU WA MAREKANI"- Rais Hassan Rouhani.
21 Sep 2020 11:51 - Grace Melleor

Rais wa Iran Hassan Rouhani amesema Marekani imeshindwa katika juhudi zake za kuiwekea tena vikwazo nchi hiyo baada ya w [ ... ]

UGANDA YAENDELEA KULEGEZA VIZUIZI DHIDI YA CORONA.
21 Sep 2020 06:31 - Grace Melleor

Rais wa Uganda Yoweri Museveni ametangaza kuwa shule na taasisi zingine za elimu ya juu, zitafunguliwa tena kuanzia mwez [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2020 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.