Star Tv

Madagascar imeuwekea mji wake mkuu Antananarivo amri ya kutotoka nje kufuatia ongezeko jipya la maambukizi ya virusi vya corona, miezi miwili baada ya masharti hayo kuondolewa.

Katika taarifa ya rais Andry Rajoelina amesema analifunga tena eneo la Analamanga ambalo ndilo lenye mji mkuu linafungwa tena, rais.

"Rais huyo amesema, 'Hakuna magari yatakayoruhusiwa kuingia ama kutoka katika eneo hilo kuanzia leo Jumatatu hadi Julai 20 na masharti makali yatawekewa wanaotoka, ni mtu mmoja mmoja katika kila familia atakayeruhusiwa kwenda barabarani kati ya saa kumi na mbili asubuhi na saa sita mchana''.

Hatua hizo zimechukuliwa kutokana na kusambaa kwa mlipuko huo na kuongezeka kwa visa vya Covid-19.

Nchi hiyo ambayo ilikuwa imezoea kuandikisha visa vichache kwa siku vya ugonjwa huo lakini sasa ,taifa hilo katika siku za hivi karibuni limethibitisha idadi kubwa ya wagonjwa wa Covid 19 kila siku , ambapo wagonjwa 216 waliripotiwa siku ya Jumamosi baada ya watu 675 kupimwa.

Mpaka kufikia sasa takribani watu 24,000 wamepimwa virusi hivyo nchini humo.

Tangu virusi hivyo vilipogunduliwa katika kisiwa hicho Machi 20, taifa hilo lilikuwa na jumla ya wagonjwa 2,728 ikiwemo watu 29 waliofariki kufikia siku ya Jumapili.

 

 

Latest News

ZIMBABWE KUKABILIANA NA WANAOIPAKA TOPE NCHI YAO.
07 Aug 2020 16:05 - Grace Melleor

Taifa la Zimbabwe limesema lipo mbioni kupitisha sheria mpya ambayo itatoa adhabu kali kwa vyama vya kisiasa vinavyofany [ ... ]

MEMBE TAYARI AJIDHATITI KWA MAPAMBANO.
07 Aug 2020 15:35 - Grace Melleor

Mgombea Urais kwa tiketi ya chama cha ACT-Wazalendo Bernard Membe tayari amechukua fomu ya kuwania Urais wa Jamhuri ya M [ ... ]

MWANAMFALME WA SAUDI ASHUTUMIWA KWA KUTUMA MAMLUKI CANADA.
07 Aug 2020 15:21 - Grace Melleor

Mwanamfalme wa Saudi Arabia Mohammed bin Salman ameshutumiwa kwa kutuma mamluki nchini Canada ili kumuua aliyekuwa afisa [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2020 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.