Rais Donald Trump amesaini sheria mpya ya kuongeza vikwazo dhidi ya Korea Kaskazini juu ya mpango wake wa nuklia.
Waziri wa fedha wa Marekani ameidhinisha vikwazo hivyo dhidi ya makampuni ya fedha yanayofanya biashara zake ndani ya Korea Kaskazini.
Rais Trump pia amesema kuwa Benki Kuu ya Uchina iliagiza benki nyingine za Uchina kuacha kufanya biashara na Korea Kaskazini.
Hatua hii inakuja katika kipindi cha chini ya wiki mbili baada ya Umoja wa Mataifa kuidhinisha vikwazo vipya dhidi ya taifa hilo kwasababu ya jaribilo lake la hivi karibuni la nuklia.