Star Tv

Waziri Mkuu wa Uingereza Liz Truss amemfuta kazi waziri wake wa fedha, Kwasi Kwarteng, muda mfupi kabla ya kiongozi huyo kupanga kuachana na hatua za kiuchumi katika jitihada za kujinusuru na misukosuko ya kisiasa inayoikabili nchi hiyo.

Truss, aliye madarakani kwa siku 37 pekee, anatathmini upya hatua za punguzo la ushuru zilizosababisha ongezeko la gharama za ukopaji na kuilazimu Benki Kuu ya Uingereza kuingilia kati.

Aidha aliyekuwa waziri wa mambo ya nje, Jeremy Hunt, ameteuliwa kuwa waziri mpya wa fedha kujaza nafasi ya Kwarteng.

Bado haijafahamika ni vipi kufutwa kazi kwa waziri huyo wa fedha kunaweza kumnusuru Truss na shinikizo kubwa dhidi yake, akilaumiwa kuwa kigeugeu kwenye utawala wake.

Latest News

Waziri Mkuu Akagua Visima Vya Dharura Dar Es Salaam
10 Nov 2022 13:31 - Kisali Shombe

¬†WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amekagua visima vya dharura vinavyosafishwa, kufufuliwa na kuunganishwa katika mfumo wa us [ ... ]

Waziri Wa Afya Aagiza Udhibiti Magonjwa Ya Mlipuko
09 Nov 2022 14:15 - Kisali Shombe

Waziri wa Afya Ummy Mwalimu ameagiza vituo vyote vya kutolea huduma za afya vya binafsi na serikali kuweka kituo maalum  [ ... ]

Vifo vitokanavyo na Utoaji wa Mimba usio salama, Kudhibitiwa
09 Nov 2022 13:21 - Kisali Shombe

Mpango wa idara ya afya wa kutoa elimu ya afya ya uzazi na matumizi ya uzazi wa mpango unatajwa kusaidia kupunguza mimba [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2023 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.