Star Tv

Rais wa Marekani Joe Biden amesema hatua ya Rais wa Urusi Vladimir Putin la kutumia silaha za nyuklia linatishia kuleta hatari kubwa kama hiyo tangu Mgogoro wa Kombora la Cuba, akiongeza kuwa Washington ilikuwa "inajaribu kubaini" njia ya Putin ya kujiondoa.

Ikulu ya White House imesema mara kwa mara kwamba haijaona dalili zozote kwamba Urusi inajiandaa kutumia silaha za nyuklia licha ya kile inachokiita "ugomvi wa nyuklia" wa Putin.
Rais Biden siku ya Alhamisi aliweka wazi kuwa alikuwa "akimwangalia Putin na jinsi anavyoweza kujibu wakati jeshi la Ukraine likipata mafanikio dhidi ya uvamizi wake".

"Kwa mara ya kwanza tangu Mgogoro wa Kombora la Cuba, tuna tishio la moja kwa moja kwa matumizi ya silaha za nyuklia, ikiwa mambo yataendelea kama yalivyokuwa,"-Rais Biden.

Aidha Biden amebainisha kwamba yeye na maafisa wa Marekani wanatafuta njia ya kidiplomasia. "Tunajaribu kufahamu ni nini njia panda ya Putin...anapata wapi njia ya kutoka? sio tu kupoteza heshima lakini kupoteza nguvu kubwa nchini Urusi,"- Biden.

#ChanzoBBC

Latest News

Waziri Mkuu Akagua Visima Vya Dharura Dar Es Salaam
10 Nov 2022 13:31 - Kisali Shombe

¬†WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amekagua visima vya dharura vinavyosafishwa, kufufuliwa na kuunganishwa katika mfumo wa us [ ... ]

Waziri Wa Afya Aagiza Udhibiti Magonjwa Ya Mlipuko
09 Nov 2022 14:15 - Kisali Shombe

Waziri wa Afya Ummy Mwalimu ameagiza vituo vyote vya kutolea huduma za afya vya binafsi na serikali kuweka kituo maalum  [ ... ]

Vifo vitokanavyo na Utoaji wa Mimba usio salama, Kudhibitiwa
09 Nov 2022 13:21 - Kisali Shombe

Mpango wa idara ya afya wa kutoa elimu ya afya ya uzazi na matumizi ya uzazi wa mpango unatajwa kusaidia kupunguza mimba [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2023 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.