Kiongozi mkuu wa Iran amezilaumu Marekani na Israel kwa kuchochea maandamano yaliyoenea nchini humo kufuatia kifo cha mwanamke mmoja aliyekuwa chini ya ulinzi wa polisi.
Katika tamko lake la kwanza hadharani kuhusu machafuko hayo, Ayatollah Ali Khamenei amesema "machafuko" yalikuwa "yamepangwa" na maadui wakubwa wa Iran na washirika wao.
Maandamano hayo ni changamoto kubwa kwa utawala wake kwa muongo mmoja, na alivitaka vikosi vya usalama kuwa tayari kwa zaidi.
Marekani imesema "imeshtushwa" na majibu ya vurugu kwa maandamano hayo.
Rais Joe Biden amesema "ana wasiwasi mkubwa" kuhusu ripoti za "kuongezeka kwa ukandamizaji wa vurugu dhidi ya waandamanaji wa amani".
Biden amesema Waandamanaji hao walikuwa wakitoa wito wa "kanuni za haki na za ulimwengu wote, "inasimama na wanawake wa Iran" ambao walikuwa "wakiuhamasisha ulimwengu kwa ushujaa wao".
Uingereza iliunga mkono kauli hizo, ikitoa wito kwa mwanadiplomasia mkuu wa Iran mjini London kuwaambia viongozi wao mjini Tehran kwamba "badala ya kuwalaumu wahusika wa nje kwa machafuko hayo, wanapaswa kuwajibika kwa matendo yao na kusikiliza kilio cha watu wao".