Mwanasheria mkuu wa zamani wa Mexico amekamatwa akihusishwa na kutoweka kwa wanafunzi 43 mwaka wa 2014.
Jesús Murillo Karam, ambaye aliongoza uchunguzi wa ukatili huo, ameshtakiwa kwa kutoweka kwa wanafunzi hao, mateso na kuzuia haki kutendeka.
Wanafunzi hao walitoweka walipokuwa wakisafiri kwa basi kupitia mji wa Iguala wakielekea kwenye maandamano katika Jiji la Mexico.
Zaidi ya vipande vya mifupa vichache vilivyopatikana kutoka kwa watatu kati yao 43, hakuna kilichoonekana wala kujulikana juu ya hatima yao.
Inaelezwa Polisi walifyatulia risasi mabasi yaliyokuwa yamewabeba wanafunzi jioni ya tarehe 26 Septemba 2014 lakini kilichotokea baadaye kimeibua mjadala.
Kutoweka kwao kwa kushangaza kulileta mshtuko kote ulimwenguni na kusababisha maandamano makubwa nchini Mexico dhidi ya vitendo vya kutokujali na kushiriki katika uhalifu.
Siku ya Alhamisi, tume iliyoundwa na Rais wa sasa Andrés Manuel López Obrador ilishutumu wanajeshi kwa kuhusika na mauaji hayo, japokuwa sio moja kwa moja bali angalau kwa uzembe.
Mapema mwaka huu Rais López Obrador alifichua kuwa wanajeshi wa wanamaji walikuwa wakichunguzwa kwa madai ya kuvuruga ushahidi, ikiwa ni pamoja na katika eneo la kutupa taka ambapo mabaki ya binadamu yalipatikana.
#ChanzoBBC