Mahakama nchini Ukraine imempatia kifungo cha maisha jela kamanda wa kitengo kimoja cha Urusi kwa kumuua raia, katika uamuzi wa kesi ya kwanza dhidi ya uhalifu wa kivita nchini humo.
Mwanajeshi huyo aliyekamatwa, sajenti Vadim Shishimarin amehukumiwa kwa kumuua Oleksandr Shelipov 62, katika Kijiji cha kaskazini mashariki cha Chupakhivka Februari 28, 2022.
Alikiri kumpiga risasi Shelipov lakini akasema alikuwa akifuata amri na kuomba radhi kwa mjane wake.
Moscow imekana kwamba wanajeshi wake waliwalenga raia wakati wa uvamizi wa taifa hilo huku Ukraine ikisema kwamba zaidi ya visa 1000 vya uhalifu wa kivita huenda vilifanyika.
#ChanzoBBC