Ukraine imekataa kusalimisha Mariupol, ikikataa ombi la Urusi la kuacha jiji hilo kufikia makataa ya saa 05:00 saa za Moscow (02:00 GMT)
Urusi ilikuwa imejitolea kuweka korido za kibinadamu ili wakazi waweze kuondoka jiji hilo
Takriban watu 300,000 wamenaswa na chakula kidogo, maji na umeme katika jiji hilo ambalo limekuwa likilipuliwa kwa bomu kwa muda wa wiki mbili zilizopita.
Urusi imeshambulia makazi kadhaa ya raia, shule, hospitali na ukumbi wa michezo. Ukraine imesema mashambulizi ya Mariupol ni uhalifu wa kivita ambao utaingia katika historia
Kulikuwa na utulivu wa saa 24 katika kupiga makombora katika miji mingi siku ya Jumapili. Lakini huko Kyiv, mji mkuu ulishuhudia mashambulizi ambayo yaliua watu wanne.
Rais wa Ukraine Zelensky pia ameikosoa Israel kwa kusitasita kutuma teknolojia yake ya ulinzi wa makombora nchini Ukraine.
Katika hotuba yake kwa bunge la Israel, alisema: “Kila mtu anajua mifumo yenu ya ulinzi ya makombora ndiyo bora zaidi… bila shaka mnaweza kuwasaidia watu wetu.