Star Tv

Baraza la jiji la Mariupol limesema kuwa vikosi vya Urusi vimeshambulia kwa mabomu shule ambayo imehifadhi watu 400 waliokuwa wakipata hifadhi ndani ya shule hiyo siku ya Jumamosi.

Maafisa wa Jeshi nchi Ukraine wameeleza kuwa jengo liliharibiwa na watu wako chini ya vifusi ambapo kuna Wanawake, watoto na wazee waliokuwa shuleni.

Rais wa Ukraine, ambaye alitoa hotuba ya video usiku wa manane ametoa tamko kuhusu mashambulizi la Urui dhidi ya jiji la Mariupol .

Rais Volodymyr Zelensky amelaani mashambulizi ya Urusi ya mara kwa mara dhidi ya Mariupol, mji wa bandari uliozingirwa na wanajeshi wa Urusi kusini-mashariki.

Amedai kuwa vikosi vya Urusi katika jiji hilo "vitaingia katika historia" kama kuwajibika kwa "uhalifu wa kivita".

Kwa zaidi ya wiki mbili sasa, jiji hilo limeshuhudia mashambulizi ya mara kwa mara ya mabomu ambayo yamekata umeme, gesi, maji ya mfereji na vifaa vingine.

Mashambulizi ya Urusi yamevunja makazi ya raia, hospitali ya watoto na uzazi, na majengo kadhaa ya makazi. Siku ya Alhamisi, bomu lilianguka kwenye ukumbi wa michezo ambapo mamia ya watu walikuwa wamekimbilia.

#ChanzoBBC

 

Latest News

Mgogoro wa Maji unatishia Amani Duniani, inasema ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa...
21 Mar 2024 14:18 - Kisali Shombe

Siku ya Maji Duniani ambayo inafanyika tarehe 22 Machi ikiwa na kaulimbiu: 'Maji kwa Ustawi na Amani. Ambapo maji ni moj [ ... ]

Matarajio katika mkutano wa BRICS nchini Afrika Kusini, Jumanne tarehe 22/2023
21 Aug 2023 12:14 - Kisali Shombe

Mkutano huo ambao utafanyikia Johannesburg nchini Afrika Kusini siku ya Jumanne, tarehe 22 Agosti 2023, unatarajiwa kuhu [ ... ]

Rais Ramaphosa Kuwa Mwenyeji wa Rais Xi Jinping wa China
21 Aug 2023 11:11 - Kisali Shombe

Rais Cyril Ramaphosa Jumanne ya tarehe 22 Agosti 2023, atakuwa mwenyeji wa Mheshimiwa Rais Xi Jinping wa China katika Zi [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2024 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.