Takriban watu 22 wafariki kufikia sasa baada ya matetemeko ya ardhi ya mfululizo kukumba magharibi mwa Afghanistan siku ya Jumatatu, maafisa walisema.
Kwa mujibu wa data kutoka Shirika la Jiolojia la Marekani (USGS), matetemeko hayo ya kipimo cha 4.9 na 5.3 yaliathiri mkoa wa kaskazini-magharibi wa Badghis, ambako na kusababisha nyumba na majengo kuporomoka.
Msemaji ameliambia shirika la habari la AFP kuwa watoto wanne ni miongoni mwa waliopatikana wamekufa kwenye vifusi.
Matetemeko ya ardhi yanaweza kusababisha uharibifu mkubwa nchini Afghanistan, ambapo makao mengi hayajaimarishwa au hayajajengwa vizuri.
USGS ilinakili matetemeko mawili ya ardhi siku ya Jumatatu, ambayo yalipiga takriban kilomita 50 (31mi) kutoka Qala-e-Naw, mji mkuu wa jimbo hilo.
Tetemeko la kwanza lilipiga alasiri, na la pili likafuata saa mbili baadaye. Athari zake zilionekana zaidi katika wilaya za Qadis na Mugr.
#ChanzoBBC