Star Tv

Mahakama ya India imemuondolea mashtaka askofu mmoja aliyeshtakiwa kwa kumbaka mtawa mmoja kati ya mwaka wa 2014 na 2016 katika kesi ambayo ilishtua jumuiya kongwe za Kikristo nchini humo.

Franco Mulakkal, mwenye umri wa miaka 54, alikamatwa kutoka jimbo la kusini la Kerala mwaka wa 2018 na alikuwa amekanusha madai hayo.

Kesi hiyo ilizua maandamano makubwa baada ya mtawa huyo kudai kuwa Kanisa Katoliki lilipuuza malalamishi yake.

Vatikani ilikuwa imemwondolea askofu kazi zake kwa muda.

Siku ya Ijumaa, mahakama ya mjini Kottayam ya Kerala ilimkuta hana hatia ya mashtaka. "Upande wa mashtaka ulishindwa kuthibitisha mashtaka yote dhidi ya mshtakiwa," alisema Jaji wa vikao vya ziada vya Kottayam (ASJ) G Gopakumar.

Mawakili wa mtawa huyo walisema watapinga uamuzi huo katika mahakama kuu.

Lakini timu ya wanasheria ya askofu huyo ilisema "imesambaratisha ushahidi wote" dhidi yake. "

Bw Mulakkal alikuwa askofu wa dayosisi ya Jalandhar katika jimbo la kaskazini la Punjab.

Mshitaki wake ni wa Wamisionari wa Yesu, huko Kerala ambalo ni sehemu ya dayosisi ya Jalandhar. A

Aidha Mtawa huyo alidai kuwa Askofu huyo alimbaka mara 13 na mashambulizi hayo yalitokea alipotembelea nyumba ya watawa alikokuwa akiishi katika jiji la Kottayam, Kerala.

#ChanzoBBC

Latest News

RAIS WA UKRAINE AAMURU RAIA WOTE KUHAMA MKOA WA DONETSK.
31 Jul 2022 17:17 - Grace Melleor

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky ameamuru raia wote ambao bado wanaishi katika maeneo ya mashariki mwa mkoa wa Donetsk [ ... ]

KIFO CHA RAIA WA NIGERIA NCHINI ITALIA CHAZUA HASIRA.
31 Jul 2022 16:58 - Grace Melleor

Kifo cha mhamiaji aliyeshambuliwa mchana kweupe nchini Italia kimezua hasira.

VUTA N’KUVUTE YA MANARA NA KATIBU WA TFF YAIBUKA.
25 Jul 2022 16:37 - Grace Melleor

Katibu Mkuu wa Shrikishi la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Kidao Wilfred amesema amesekitishwa na madai ya yaliyekuwa Af [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2022 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.