Star Tv

Waziri Mkuu wa kwanza mwanamke kuwahi kushikilia wadhifa huo nchini Sweden amejiuzulu saa chache mara baada ya kuteuliwa.

Magdalena Andersson, alitangazwa kama kiongozi Jumatano, lakini alijiuzulu baada chama kishiriki katika muungano wake kujiuzulu serikalini na bajeti yake kushindwa kupitishwa.

Badala yake, bunge lilipigia kura bajeti iliyoandaliwa na upinzani ambayo ilijumuisha mpango wa mrengo wa kulia zaidi wa kupinga uhamiaji.

"Nimemwambia spika kwamba ningependa kujiuzulu"-Bi Andersson aliwaambia waandishi wa habari.

Mshirika wake katika muungano, chama cha kijani (Green Party) kilisema kuwa kuwa hakikuweza kuikubali bajeti "iliyoandaliwa kwa mara ya kwanza na chama cha upinzani cha mrengo wa kulia zaidi ".

Aidha, Bi Andersson amesema kwamba ana matumaini ya kujaribu kuwa waziri mkuu tena wakati mwingine kama kiongozi wa serikali wa chama kimoja.

#ChanzoBBCSwahili

Latest News

MATETEMEKO MAWILI YA ARDHI YAUA WATU 22 AFGHANISTAN.
18 Jan 2022 09:36 - Grace Melleor

Takriban watu 22 wafariki kufikia sasa baada ya matetemeko ya ardhi ya mfululizo kukumba magharibi mwa Afghanistan siku  [ ... ]

WAZIRI MKUU AWATAKA MABALOZI KUVUTIA WAWEKEZAJI.
17 Jan 2022 16:24 - Grace Melleor

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewataka mabalozi wanaoiwakilisha Tanzania katika mataifa mbalimbali watoe msukumo Katika u [ ... ]

RAIS WA MALI ALIYEPENDULIWA MADARAKANI AFARIKI.
17 Jan 2022 06:53 - Grace Melleor

Rais wa Mali aliyeondolewa madarakani Ibrahim Boubacr Keita amefariki akiwa na umri wa miaka 76, familia yake na rafiki  [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2022 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.