Star Tv

Takriban watu milioni mbili ambao hawajachanjwa kikamilifu dhidi ya Covid-19 wamewekwa chini ya zuio la kutotoka nje nchini Austria huku nchi hiyo ikikabiliwa na kuongezeka kwa visa vya ugonjwa huo.

Watu ambao hawajachanjwa wataruhusiwa tu kuondoka nyumbani kwa sababu chache, kama vile kufanya kazi au kununua chakula.

"Hatuchukui hatua hii kirahisi, lakini kwa bahati mbaya ni muhimu," Kansela Alexander Schallenberg alisema.

Takriban 65% ya wakazi wa Austria wamechanjwa kikamilifu mojawapo ya viwango vya chini kabisa Ulaya Magharibi.

Wakati huohuo, kiwango cha maambukizi ya siku saba ni zaidi ya kesi 800 kwa kila watu 100,000, ambayo ni moja ya juu zaidi barani Ulaya.

Kwa ujumla, Ulaya imekuwa tena eneo lililoathiriwa zaidi na janga hili na nchi kadhaa zinaanzisha vizuizi na onyo la kuongezeka kwa visa vya ugonjwa huo.

#ChanzoBBC

Latest News

MATETEMEKO MAWILI YA ARDHI YAUA WATU 22 AFGHANISTAN.
18 Jan 2022 09:36 - Grace Melleor

Takriban watu 22 wafariki kufikia sasa baada ya matetemeko ya ardhi ya mfululizo kukumba magharibi mwa Afghanistan siku  [ ... ]

WAZIRI MKUU AWATAKA MABALOZI KUVUTIA WAWEKEZAJI.
17 Jan 2022 16:24 - Grace Melleor

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewataka mabalozi wanaoiwakilisha Tanzania katika mataifa mbalimbali watoe msukumo Katika u [ ... ]

RAIS WA MALI ALIYEPENDULIWA MADARAKANI AFARIKI.
17 Jan 2022 06:53 - Grace Melleor

Rais wa Mali aliyeondolewa madarakani Ibrahim Boubacr Keita amefariki akiwa na umri wa miaka 76, familia yake na rafiki  [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2022 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.