Wawakilishi wa mataifa duniani wanaokutana mjini Glasgow kwa mkutano wa kimataifa wa mabadiliko ya tabia ya nchi wa COP26 wametumia siku ya Jumamosi kupigania uwezekano wa kufikia mkataba.
Kwa karibu siku nzima wajumbe hao wamekuwa wakijadili mapendekezo mapya yanayonuwia kupatikana kwa mkataba utakaotanua juhudi za ulimwengu katika kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.
Maafisa wa Uingereza wanaoongoza majadiliano mjini Glasgow, Scotland walitoa rasimu mpya makubaliano baada ya juhudi chungunzima za kidiplomasia zilizoendelea hadi siku ya Ijumaa ambayo ndiyo ilikuwa ya mwisho ili kufikiwa makubaliano.
Baadhi ya makundi ya wanaharakati wa mazingira yamesema mapendekezo yaliyo mezani hivi sasa kwa wajumbe kuamua hayana uzito wa kutosha.
#ChanzoDW