Star Tv

Waendesha mashtaka wa Ufaransa wamefungua uchunguzi kuhusu madai ya ubakaji katika ikulu ya rais mjini Paris.

Vyombo vya habari nchini humo vinaripoti kwamba mwanajeshi wa kike amesema alinajisiwa baada ya tafrija ya vinywaji katika jumba la Élysée mwezi Julai.

Rais Emmanuel Macron alikuwa amehudhuria hafla hiyo, iliyofanyika kwa wafanyakazi wanaoondoka.

Mtuhumiwa pia mwanajeshi ambaye amehojiwa, lakini bado hajafunguliwa mashtaka rasmi, ripoti zinasema.

Gazeti la Libération liliripoti kwanza mashtaka hayo siku ya Ijumaa.

Wote wawili wanaodaiwa kuwa mwathiriwa na mshambulizi waliripotiwa kufanya kazi katika ofisi ya wafanyakazi wa ulinzi mkali katika jengo hilo, na Libération ilisema wanafahamiana.

Afisa wa rais aliliambia shirika la habari la AFP kwamba "mara tu mamlaka zilipofahamu madai haya, hatua zilichukuliwa mara moja" kumsaidia mwathiriwa huyo.

Aidha mwathiriwa wa tukio hilo na mtuhumiwa wote wamehamishwa katika majukumu mengine, ikulu ilisema.

Latest News

RAIS WA UKRAINE AAMURU RAIA WOTE KUHAMA MKOA WA DONETSK.
31 Jul 2022 17:17 - Grace Melleor

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky ameamuru raia wote ambao bado wanaishi katika maeneo ya mashariki mwa mkoa wa Donetsk [ ... ]

KIFO CHA RAIA WA NIGERIA NCHINI ITALIA CHAZUA HASIRA.
31 Jul 2022 16:58 - Grace Melleor

Kifo cha mhamiaji aliyeshambuliwa mchana kweupe nchini Italia kimezua hasira.

VUTA N’KUVUTE YA MANARA NA KATIBU WA TFF YAIBUKA.
25 Jul 2022 16:37 - Grace Melleor

Katibu Mkuu wa Shrikishi la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Kidao Wilfred amesema amesekitishwa na madai ya yaliyekuwa Af [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2022 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.