Star Tv

Mwanamke mmoja amejifungua watoto saba mjini Abbottabad huko Pakistan.

"Mungu ametujalia watoto wanne wa kiume na watatu wa kike. Tunafuraha sana". - Alisema mume wake, Yar Mohammad

Kulingana na vyanzo vya habari katika hospitali hiyo, hali ya watoto hao na mama yao imeimarika.

Bwana Mohammed anasema uchunguzi wa awali ulipobaini mke wake amebeba watoto kadhaa tumboni walishauriwa waende hospitali kuu kwa uangaalizi wa karibu.

Madaktaktari waliomhudumia walishangazwa sana na hali ya mwanamke huyo.

Kulingana na Dkt Hina Fayaz, daktari bingwa wa wanawake katika Hospitali ya Jinnah huko Abbottabad, mwanamke huyo alikuja kwake kwa mara ya kwanza Jumamosi.

Anasema, "Baada ya uchunguzi wa ultrasound na ripoti zingine, tuligundua kuwa ana watoto watano ndani ya tumbo lake na ujauzito wake ulikua zaidi ya miezi minane".

Dkt. Hina Fayaz anasema kwamba alishtuka sana kuona ripoti ya matibabu ya mwanamke huyo aliyejifungua watoto saba.

#ChanzoBBCSwahili

Latest News

SHAMBULIO LA KUJITOA MHANGA LAUA WATU NANE SOMALIA.
25 Nov 2021 10:26 - Grace Melleor

Polisi nchini Somalia wamethibitisha vifo vya raia katika bomu lililotegwa ndani ya gari katika mji mkuu Mogadishu, tele [ ... ]

WAZIRI MKUU SWEDEN AJIUZULU SAA CHACHE BAADA YA KUTEULIWA.
25 Nov 2021 09:01 - Grace Melleor

Waziri Mkuu wa kwanza mwanamke kuwahi kushikilia wadhifa huo nchini Sweden amejiuzulu saa chache mara baada ya kuteuliwa [ ... ]

MTOTO WA GADDAFI AZUIWA KUGOMBEA URAIS LIBYA.
25 Nov 2021 07:13 - Grace Melleor

Mtoto wa aliyekuwa kiongozi wa Libya hayati Muammar Gaddafi ameenguliwa katika kinyang’anyiro cha kuwania uchaguzi wa  [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2021 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.