Star Tv

Shirika la Afya Duniani limesema limesikitishwa na madai ya unyanyasaji wa ngono unaofanywa na wafanyakazi wake nchini DRC wakati wa mlipuko wa Ebola.

Madai hayo ambayo yalikuja, mwaka mmoja baada ya uchunguzi uliofanywa na shirika la habari za masuala ya kibinadamu na taasisi ya Thomson Reuters.

Wanawake wa eneo hilo walidai kunyweshwa pombe, kuviziwa na kulazimishwa kufanya ngono na wawili walipata ujauzito.

Mkurugenzi wa WHO barani Afrika, Matshidiso Moeti ameomba radhi kwa wanawake na wasichana waliopata masaibu hayo kwa mwaka 2018 na 2020 kwasababu hatua kali zitachukuliwa kwa wafanyakazi hao na watumishi wengine wa afya.

Wachunguzi huru wanasema kuwa mfumo umeshindwa na uzembe wa mtu mmoja katika ripoti yao.

Katibu mkuu wa WHO Tedros Adhanom Ghebreyesus alisema ripoti hiyo inafadhaisha kuisoma.

Aliomba radhi na kuongeza kuwa hataacha kuahidi kuwasaidia waathirika kwa ulinzi na kupata haki yao.

Latest News

UFARANSA YAZINDUA MAGARI YA UMEME HAPA NCHINI.
20 Oct 2021 15:31 - Grace Melleor

Waziri wa Biashara na uchumi nchini Ufaransa Franck Riester amezindua magari ya umeme yaliyoundwa na kampuni ya E-Motion [ ... ]

UHITAJI WA NYAMA WAONGEZEKA NCHINI.
20 Oct 2021 15:23 - Grace Melleor

Serikali imesema malalamiko yaliyojitokeza hivi karibuni ya kupanda kwa bei ya nyama nchini yanaashiria ukuaji wa sekta  [ ... ]

UGANDA YAZINDUA GARI LA KIVITA LILILOUNDWA NCHINI HUMO.
19 Oct 2021 18:03 - Grace Melleor

Jeshi la Uganda limezindua gari la kivita lililoundwa nchini humo.

Other Articles

Social Media

Copyright © 2021 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.