Star Tv

Chama cha Rais Vladimir Putin cha United Russia party kinaonekana kupata ushindi mkubwa wa wabunge, huku kukiwa madai ya wizi wa kura.

Kura za awali zinatoa utabiri mkubwa wa ushindi kwa chama tawala.

Wakosoaji wengi wa Kremlin walizuiwa kushiriki katika uchaguzi huo, na kumekuwa na ripoti kadhaa za kura kuibwa na wengine kulazimishwa kupiga kura.

Tume ya uchaguzi ilikataa madai hayo na kura zilizopigwa zimeweza kuchagua wabunge 450 kwa bunge la Duma huko Moscow ambapo jumla ya vyama 14 vilikuwa sehemu ya kura hiyo.

Katika matokeo ya awali , tume ilisema kwamba 50% ya kura zilizohesabiwa, chama cha United Russia kimepata zaidi ya kura 46%, kikifuatiwa na Chama cha Communist party kwa 21%

United Russia ilidai kushinda saa chache baada ya vituo vya kupigia kura kufungwa Jumapili jioni.

Televisheni ya taifa ilionesha ofisa wa juu wa United Russia , Andrei Turchak, akiwapongeza wafuasi wake huko Moscow kwa kile alichokuwa akikifafanua kuwa ushindi wa haki na kweli .

Matokeo ya awali yanaonesha kuwa licha ya kwamba chama cha Putin kinaweza kuwa na viti vingi bungeni , ambapo imepoteza kama moja ya tano ya wafuasi wake.

Mwaka 2016, chama hicho kilipata ushindi wa 54% ya kura. Chama cha Communists kiliona wafuasi wao waliongezeka kwa 8%.

#ChanzoBBCSwahili

Latest News

UFARANSA YAZINDUA MAGARI YA UMEME HAPA NCHINI.
20 Oct 2021 15:31 - Grace Melleor

Waziri wa Biashara na uchumi nchini Ufaransa Franck Riester amezindua magari ya umeme yaliyoundwa na kampuni ya E-Motion [ ... ]

UHITAJI WA NYAMA WAONGEZEKA NCHINI.
20 Oct 2021 15:23 - Grace Melleor

Serikali imesema malalamiko yaliyojitokeza hivi karibuni ya kupanda kwa bei ya nyama nchini yanaashiria ukuaji wa sekta  [ ... ]

UGANDA YAZINDUA GARI LA KIVITA LILILOUNDWA NCHINI HUMO.
19 Oct 2021 18:03 - Grace Melleor

Jeshi la Uganda limezindua gari la kivita lililoundwa nchini humo.

Other Articles

Social Media

Copyright © 2021 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.