Star Tv

Kiongozi wa Algeria ametangaza siku tatu za maombolezo kuanzia leo hii, kufuatia kifo cha Rais wa zamani wa taifa hilo, Abdelaziz Bouteflika.

Rais huyo wa zamani wa Algeria, Abdelaziz Bouteflika, amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 84 baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Bouteflika ambaye utawala wake wa miaka 20, unatajwa kugubikwa na rushwa na aliondoshwa madarakani kwa maandamano makubwa baada ya kutaka kugombea madaraka kwa muhula mpya.

Bouteflika aliyefikwa na maradhi ya kiharusi mwaka 2013, alifariki dunia Ijumaa, akiwa na umri wa miaka 84.

Katika siku zake za mwisho za urais wake alikuwa akionekana kwa nadra sana.

Rais huyo zamani hajaonekana kabisa hadharani tangu, Rais Abdelmadjid Tebboune achukue hatamu ya uongozi wa Algeria.

Ofisi ya rais huyo wa sasa imesema katika maombolezo hayo ya siku 3 bendera zitapepea kwa nusu mlingoti.

Latest News

UFARANSA YAZINDUA MAGARI YA UMEME HAPA NCHINI.
20 Oct 2021 15:31 - Grace Melleor

Waziri wa Biashara na uchumi nchini Ufaransa Franck Riester amezindua magari ya umeme yaliyoundwa na kampuni ya E-Motion [ ... ]

UHITAJI WA NYAMA WAONGEZEKA NCHINI.
20 Oct 2021 15:23 - Grace Melleor

Serikali imesema malalamiko yaliyojitokeza hivi karibuni ya kupanda kwa bei ya nyama nchini yanaashiria ukuaji wa sekta  [ ... ]

UGANDA YAZINDUA GARI LA KIVITA LILILOUNDWA NCHINI HUMO.
19 Oct 2021 18:03 - Grace Melleor

Jeshi la Uganda limezindua gari la kivita lililoundwa nchini humo.

Other Articles

Social Media

Copyright © 2021 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.