Star Tv

Raia wa Marekani wameadhimisha miaka 20 hii leo tangu kutokea mashambulizi mabaya ya kigaidi Septemba 11 mwaka 2001.

Kengele zilisikika katika maeneo ya makumbusho mjini New York, Penn-sylvania, na Pentagon huku watu wakinyamaza kimya kwa dakika moja kuwakumbuka walioangamia katika mkasa huo.

Ndege ya kwanza iliyokuwa na magaidi wanne ilianguka katika jengo la maghorofa pacha la kituo cha kimataifa cha biashara mjini New York lililoporomoka wakati huo.

Marais wa zamani Barrack Obama na Bill Clinton ni miongoni mwa wageni waliohudhuria kumbukumbu za shambulio hilo mjini New York.

Rais wa Marekani Joe Biden ameyatembelea maeneo matatu yaliyoshambuliwa mnamo 9/11- mwaka 2001 huku viongozi wa ulimwengu wakiendelea kutuma ujumbe kwa kiongozi huyo na watu wa Marekani.

Rais Biden amesema umoja wa kitaifa ndiyo nguvu kubwa kabisa ya Marekani, katika ujumbe wake wa kumbukumbu ya miaka 20, tangu mashambulizi ya kigaidi ya Septemba 11.

Biden amesema pamoja na hisia kali za umoja wa kitaifa, baada ya tarehe 11 Septemba 2001, Marekani imeshuhudia pia ushujaa kila mahali.

Mashambulio hayo ya kigaidi ya Septemba 11, mnamo mwaka 2001 yalisababisha vifo vya watu 2,977.

Clifford Chanin makamu mtendaji mkuu wa ukumbi wa Makumbusho ya Kitaifa ya Septemba 11 uliojengwa katika eneo la shambulio kwenye Kituo cha Biashara Ulimwenguni, (World Trade Center) amesema maadhimisho hayo yatatafakari hisia nyingi kwa nchi hiyo kwa kuzingatia wapi wamarekani walipo, wapi walipokuwa na wanakoelekea.

Mashambulizi hayo ya kigaidi kwa kutumia ndege za abiria, ndiyo pekee yaliyowahi kufanywa na maadui wa kigeni ndani ya ardhi ya Marekani, katika historia ya taifa hilo lenye nguvu kubwa za kijeshi ulimwenguni, na iliyatumia kama sababu ya kuvamia Afghanistan na Iraq.

Kumbukumbu ya 9/11 ya mwaka huu inafanyika ikiwa ni muda mfupi tangu Marekani kumaliza uwepo wa majeshi yake nchini Afghanistan, ambayo yalikuweko miaka 20 iliyopita kwa ajili ya kupambana na magaidi wa kundi la Al-Qaeda, ambalo lilifanya mashambulio ya 9/11 nchini Marekani mnamo mwaka 2001.

#ChanzoDWSwahili

Latest News

Mgogoro wa Maji unatishia Amani Duniani, inasema ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa...
21 Mar 2024 14:18 - Kisali Shombe

Siku ya Maji Duniani ambayo inafanyika tarehe 22 Machi ikiwa na kaulimbiu: 'Maji kwa Ustawi na Amani. Ambapo maji ni moj [ ... ]

Matarajio katika mkutano wa BRICS nchini Afrika Kusini, Jumanne tarehe 22/2023
21 Aug 2023 12:14 - Kisali Shombe

Mkutano huo ambao utafanyikia Johannesburg nchini Afrika Kusini siku ya Jumanne, tarehe 22 Agosti 2023, unatarajiwa kuhu [ ... ]

Rais Ramaphosa Kuwa Mwenyeji wa Rais Xi Jinping wa China
21 Aug 2023 11:11 - Kisali Shombe

Rais Cyril Ramaphosa Jumanne ya tarehe 22 Agosti 2023, atakuwa mwenyeji wa Mheshimiwa Rais Xi Jinping wa China katika Zi [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2024 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.