Star Tv

Mlipuko wa ugonjwa wa uti wa mgongo au meningitis umetangazwa kuua watu 120 Kaskazini mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Imethibitishwa kuwa mpaka sasa watu zaidi ya 120 wamekufa kutokana na ugonjwa huo.

Mgonjwa wa kwanza nchini DRC aliripotiwa Julai.

Mlipuko huo umekuwa mgumu kukabiliana nao kwa kuwa jamii inauhusisha na uchawi, shirika la afya duniani (WHO) limeiambia BBC.

Sampuli zilizotumwa Ufaransa zimebaini kuwa bakteria wanaohusika na mlipuko huo wanaweza kusababisha janga kubwa.

Watu wengi wamekufa na jamii inapaswa kulaumiwa kwa kushindwa kuwajibika, kwakuwa badala ya kutafuta tiba, baadhi ya watu wamekuwa wakitoka sehemu moja kwenda nyingine wakiwa na matumaini kuwa ugonjwa huo hautawafuata.

Serikali ya DRC na WHO wametuma vikosi vya watumishi wa afya kaskazini mashariki mwa jimbo la Tshopo ili kukabiliana na hali hiyo.

 

 

Latest News

UFARANSA YAZINDUA MAGARI YA UMEME HAPA NCHINI.
20 Oct 2021 15:31 - Grace Melleor

Waziri wa Biashara na uchumi nchini Ufaransa Franck Riester amezindua magari ya umeme yaliyoundwa na kampuni ya E-Motion [ ... ]

UHITAJI WA NYAMA WAONGEZEKA NCHINI.
20 Oct 2021 15:23 - Grace Melleor

Serikali imesema malalamiko yaliyojitokeza hivi karibuni ya kupanda kwa bei ya nyama nchini yanaashiria ukuaji wa sekta  [ ... ]

UGANDA YAZINDUA GARI LA KIVITA LILILOUNDWA NCHINI HUMO.
19 Oct 2021 18:03 - Grace Melleor

Jeshi la Uganda limezindua gari la kivita lililoundwa nchini humo.

Other Articles

Social Media

Copyright © 2021 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.