Star Tv

Japan imezuia matumizi ya chanjo ya Moderna ya Covid-19 baada ya chembechembe zisizo za kawaida kupatikana ndani ya chupa moja ya chanjo hiyo.

Mfamasia mmoja aliona chembechembe kadhaa nyeusi kwenye chupa moja ya chanjo hiyo katika Jimbo la Kanagawa, kulingana na mamlaka.

Watu wengine 3,790 walikuwa tayari wamepokea chanjo hiyo, na sasa hivi chanjo iliyosalia imezuiwa kutumika tena.

Hatua hii inachukuliwa chini ya wiki moja baada ya Japani kusimamisha utumiaji wa dozi milioni 1.63 za chanjo ya Moderna kwasababu ya uchafuzi.

Mfamasia alipata chembechembe nyeusi wakati akiangalia kama kuna chochote kisicho cha kawaida ndani ya chanjo kabla ya matumizi.

Aidha, msambazaji wa chanjo hiyo amekusanya ile inayoshukiwa kuwa na uchafu.

Ripoti za vyombo vya habari, zinasema hakuna ushahidi hadi sasa wa hatari zozote za kiafya zinazoweza kusababishwa na chanjo iliyochafuliwa.

Duka la kuuza dawa la Takeda, ambalo linauza na kusambaza chanjo hiyo huko Japani, ilikuwa tu wiki iliyopita lilipozuia matumizi ya makundi matatu ya chanjo hiyo baada ya kupatikana kwa, "chembe chembe’’- katika dozi kadhaa za kundi la vichupa 560,000.

Kampuni ya dawa ya Uhispania Rovi, ambayo huweka chanjo hiyo kwenye vichupa, ilisema katika taarifa kwamba njia ya utengenezaji nchini Uhispania inaweza kuwa sababu ya hilo na kuongeza kuwa ilikuwa ikifanya uchunguzi.

Siku ya Jumanne, waziri wa afya wa Japan alisema madai ya namna hiyo katika mkoa wa kusini wa Okinawa yalitokana na sindano kuingizwa visivyo kwenye vichupa vyenye chanjo.

Japan inapambana na kiwango kikubwa cha maambukizi ya virusi vya corona wakati ambapo ni mwenyeji wa Michezo ya Walemavu, Paralimpiki.

#ChanzoBBCSwahili

Latest News

Mgogoro wa Maji unatishia Amani Duniani, inasema ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa...
21 Mar 2024 14:18 - Kisali Shombe

Siku ya Maji Duniani ambayo inafanyika tarehe 22 Machi ikiwa na kaulimbiu: 'Maji kwa Ustawi na Amani. Ambapo maji ni moj [ ... ]

Matarajio katika mkutano wa BRICS nchini Afrika Kusini, Jumanne tarehe 22/2023
21 Aug 2023 12:14 - Kisali Shombe

Mkutano huo ambao utafanyikia Johannesburg nchini Afrika Kusini siku ya Jumanne, tarehe 22 Agosti 2023, unatarajiwa kuhu [ ... ]

Rais Ramaphosa Kuwa Mwenyeji wa Rais Xi Jinping wa China
21 Aug 2023 11:11 - Kisali Shombe

Rais Cyril Ramaphosa Jumanne ya tarehe 22 Agosti 2023, atakuwa mwenyeji wa Mheshimiwa Rais Xi Jinping wa China katika Zi [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2024 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.