Star Tv

Waziri Mkuu mpya wa Israel Naftali Bennett ameapa kuliunganisha taifa hilo ambalo linalezwa kufadhaishwa na chaguzi nne katika kipindi cha miaka miwili ya kukwama kisiasa.

Waziri Bennett amesema serikali yake itafanya kazi kwa ajili ya watu wote na vipaumbele atakavyovitoa ni katika mageuzi ya elimu, afya pamoja na kupunguza taratibu nyingi za serikali.

Waziri huyo wa mrengo wa kulia ataongoza muungano ambao haujawahi kutokea wa vyama vinavyoungwa mkono na wabunge katika kura ya Jumapili iliyoishia 60-59.

Bwana Bennett, kiongozi wa chama cha Yamina, atakuwa waziri mkuu hadi Septemba 2023 kama sehemu ya makubaliano ya kugawana madaraka, amemrithi Benjamin Netanyahu ambaye alilazimishwa kuondoka ofisini baada ya miaka 12.

Bwana Netanyahu - waziri mkuu wa Israeli aliyehudumu kwa muda mrefu zaidi - atabaki kuwa mkuu wa chama cha mrengo wa kulia cha Likud na kuwa kiongozi wa upinzani.

Katika hotuba yake, Bwana Bennett, 49, alisema; "Hii sio siku ya maombolezo, Kuna mabadiliko ya serikali katika demokrasia".

Aidha, wawakilishi nchini Palestina wametoa maoni kuhusu serikali mpya ya Israeli; "Hili ni jambo la ndani la Israeli. Msimamo wetu umekuwa wazi kila wakati, tunachotaka ni serikali ya Palestina kwenye mipaka ya 1967 na Jerusalem kama mji mkuu wake"-Msemaji wa Rais wa Palestina Mahmoud Abbas alisema.

Rais wa Marekani Joe Biden alituma pongezi zake kwa Bwana Bennett, akisema anatarajia kuimarisha uhusiano wa karibu na wa kudumu baina ya taifa la Marekani na Palestina.

Bwana Netanyahu amehudumu kwa rekodi ya mihula mitano , mara ya kwanza kuanzia mwaka 1996 hadi 1999, na baadaye kuendelea kutoka mwaka 2009 hadi 2021.

Latest News

“MAISHA HAYAJI MARA MBILI, TUSIPOTOSHE KUHUSU CHANJO”-IGP. Simon Sirro.
29 Jul 2021 11:30 - Grace Melleor

Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP. Simon Sirro, amewataka Wananchi na Watanzania kwa ujumla wasidanganywe na watu wacha [ ... ]

“MIMI NI MAMA, BIBI, MKE NA RAIS, SIWEZI KUJIWEKA KATIKA HATARI”-Rais Samia....
28 Jul 2021 10:26 - Grace Melleor

Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amepokea chanjo dhidi ya Ugonjwa wa COVID-19, Ambayo ameizindua leo Julai 28, Katik [ ... ]

MSICHANA AUAWA KWA KUVAA JEANS.
28 Jul 2021 09:51 - Grace Melleor

Msichana mmoja aliyejulikana kwa jina la Neha Paswan, mwenye umri wa miaka 17, anadaiwa kupigwa hadi kufa na watu wa fam [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2021 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.