Star Tv

Rafiki wa zamani wa Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amesema anataka kuunda serikali ya muungano na upinzani nchini humo, hiyo ikiwa ni hatua kubwa katika kuufikisha mwisho utawala wa muda mrefu wa waziri huyo mkuu.

Tangazo hilo la Naftali Bennett, ambaye ni kiongozi wa chama kidogo cha Yamina, limetoa nafasi ya msururu wa hatua ambazo huenda zikamsukuma Netanyahu na chake cha Likud katika upinzani wiki ijayo. "Serikali itafanikiwa iwapo tu tutashirikiana kama kikundi. Sio mimi bali sisi. Tutarudisha neno "sisi" ambalo ndilo lililokuwa silaha ya siri ya Israel tangu siku ya kwanza. Vyama vyote vinaalikwa kuungana na serikali."Huku Bennett na washirika wake wapya wakiongozwa na kiongozi wa upinzani Yair Lapid wakiwa bado wana vigingi vingi mbele yao, pande hizo zinaonekana kuwa zimedhamiria kupata makubaliano. Makubaliano hayo yataufikisha mwisho mkwamo ambao umeipelekea nchi hiyo kushuhudia chaguzi nne katika kipindi cha miaka miwili iliyopita.

CHANZO: IDHAA YA KISWAHILI (DW).

Latest News

WATANZANIA WATAKIWA KUENDELEA KULIPA KODI BILA KUCHOKA.
14 Jun 2021 19:01 - Grace Melleor

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amewataka watanzania kuendelea kujitoa kulipa kodi ili kuwez [ ... ]

WAZIRI MKUU MPYA AAPA KUIUNGANISHA ISRAEL.
14 Jun 2021 06:33 - Grace Melleor

Waziri Mkuu mpya wa Israel Naftali Bennett ameapa kuliunganisha taifa hilo ambalo linalezwa kufadhaishwa na chaguzi nne  [ ... ]

RAIS SAMIA AZINDUA KIWANDA CHA KUSAFISHA DHAHABU NA JENGO LA BOT.
13 Jun 2021 14:11 - Grace Melleor

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amezindua kiwanda cha kusafisha dhahabu jijini Mwanza kinach [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2021 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.