Star Tv

Rais wa Syria Bashar al-Assad ameshinda muhula wa nne madarakani kwa kupata asilimia 95.1 ya kura zote zilizopigwa.

Vyama vya upinzani Syria pamoja na mataifa ya Magharibi vimemkosoa Assad na kusema kwamba uchaguzi huo ulitawaliwa na udanganyifu.

Serikali ya Assad imesema uchaguzi uliofanywa Jumatano unaonyesha kwamba Syria inaendesha shughuli zake kikamilifu licha ya mgogoro wa mwongo mzima.

Vita hivyo vimesababisha vifo vya mamia kwa maelfu ya watu na wengine milioni 11 ambao ni nusu ya idadi ya watu kupoteza makazi yao.

Spika wa bunge Hammouda Sabbagh alitangaza matokeo katika mkutano wa waandishi wa habari jana, na kusema kwamba asilimia 78 ya watu walijitokeza kupiga kura ambayo ni zaidi ya Wasyria milioni 14.
#ChanzoDWSwahili

Latest News

Mgogoro wa Maji unatishia Amani Duniani, inasema ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa...
21 Mar 2024 14:18 - Kisali Shombe

Siku ya Maji Duniani ambayo inafanyika tarehe 22 Machi ikiwa na kaulimbiu: 'Maji kwa Ustawi na Amani. Ambapo maji ni moj [ ... ]

Matarajio katika mkutano wa BRICS nchini Afrika Kusini, Jumanne tarehe 22/2023
21 Aug 2023 12:14 - Kisali Shombe

Mkutano huo ambao utafanyikia Johannesburg nchini Afrika Kusini siku ya Jumanne, tarehe 22 Agosti 2023, unatarajiwa kuhu [ ... ]

Rais Ramaphosa Kuwa Mwenyeji wa Rais Xi Jinping wa China
21 Aug 2023 11:11 - Kisali Shombe

Rais Cyril Ramaphosa Jumanne ya tarehe 22 Agosti 2023, atakuwa mwenyeji wa Mheshimiwa Rais Xi Jinping wa China katika Zi [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2024 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.