Mji Mkuu wa Somalia Mogadishu, Jumatatu hii umeripotiwa kuwa shwari baada ya mapigano kati ya wanaounga mkono upinzani na vikosi vya usalama vya serikali, Redio binafsi ya Risala imeripoti.
Mapigano makali kati ya wapiganaji watiifu wa upinzani na vikosi vya usalama vya serikali yalizuka siku ya Jumapili.
''Hali katika maeneo yaliyotokea mapigano yamekuwa shwari hii leo na watu walionekana wakitembea katika maeneo yao ya kazi na wengine walitoka kwa ajili ya kutathimini hali ilivyo'' -tovuti ya Redio ya Risala imeeleza.
Mapigano yamezuka katika mji mkuu wa Somalia Mogadishu kati ya makundi kinzani ya vikosi vya usalama nchini humo.
Ripoti zinasema kwamba silaha kali zilitumika huku makombora yakirushwa karibu na kasri la rais.
Baadhi ya vikosi hivyo vinamuunga rais Mohammed Abdaullahi Mohammed huku vingine vikimpinga.
Wiki iliyopita bwana Mohammed anayejulikana kama Farmajo kwa utata alijiongezea muda wake ofisini, Muhula wake uliisha rasmi mwezi Februari.