Star Tv

Mfanyakazi wa hospitali nchini Italia ameshutumiwa kwa kuacha kazi huku akiwa anaendelea kupokea malipo kamili ya mshahara kwa miaka 15, ripoti vyombo vya habari nchini humo vimeripoti.

Mfanyakazi huyo ambaye ni mwanamume alikuwa mtumishi wa serikali, na anadaiwa kuacha kuripoti kazini katika hospitali ya Ciaccio Kusini mwa jiji la Catanzaro mnamo 2005.

Mfanyakazi huyo kwa sasa anachunguzwa kwa ulaghai, wizi na utumizi mbaya wa ofisi, shirika la habari la habari la Italia Ansa limeripoti.

Inasemekana alilipwa € 538,000 (Pauni 464,000) kwa jumla kwa miaka ambayo hakuwa akifanya kazi.

Mameneja sita katika hospitali hiyo pia wanachunguzwa kuhusiana na tukio hilo.

Kukamatwa kwake ni matokeo ya uchunguzi wa muda mrefu wa polisi juu kuhusu tabia ya watu kukwepa kufanya kazi na udanganyifu katika sekta ya umma ya Italia.

Ilikuwa ni wakati huo ambapo aliacha kwenda kazini, polisi walisema. Polisi pia wamemtuhumu kwa kumtishia Meneja wake kumzuia kumchukulia hatua za kinidhamu Meneja huyo ambaye baadaye alistaafu.

Aidha, polisi iliongeza kuwa kutokuwepo kwake hakukuwahi kugunduliwa na aliyechukua nafasi yake au idara ya kusimamia wafanyakazi wenzake.

Chanzo:BBCSwahili

Latest News

“TUTAJIRIDHISHA KABLA YA KUKUBALI CHANJO YA CORONA”- Rais Samia.
14 May 2021 18:24 - Grace Melleor

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amesema kabla ya kupokea chanjo ya virusi vya Corona ni lazi [ ... ]

SOMALIA YATANGAZA KUREJESHA UHUSIANO NA KENYA.
06 May 2021 17:57 - Grace Melleor

Somalia imetangaza kuwa inarejesha mahusiano ya kidiplomasia na nchi jirani ya Kenya baada ya kusitisha mahusiano hayo m [ ... ]

KENYA NA TANZANIA KUONDOA VIKWAZO VYA BIASHARA.
05 May 2021 15:39 - Grace Melleor


Rais Samia Suluhu Hassan amesema Tanzania iko tayari kuwapokea wawekezaji kutoka Kenya pamoja na kuondoa vikwazo visivy  [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2021 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.