Star Tv

Kampuni yenye makao yake nchini Lesotho imeruhusiwa kuuza mazao ya bangi kwa ajili ya matumizi ya dawa kwa Muungano wa Ulaya.

Kampuni hiyo kwa jina, MG Health, imesema kwamba imepokea uthibitisho rasmi kwamba mchakato wake wa utengenezaji unakidhi viwango vya uzalishaji vya Muungano wa Ulaya.

Kampuni hiyo inakuwa ya kwanza barani Afrika kuuza bangi kwa ajili ya dawa kwa Muungano wa Ulaya.

"Kile ambacho hii inamaanisha ni kwamba tuna idhini ya kuuza bidhaa zetu kama API [kiungo cha kifamasia] ndani ya Ujerumani, na soko pana la Muungano wa Ulaya . Tunatarajia kuanza mwezi Juni," -Shirika la habari la Reuters lilimnukuu Mkurugenzi mkuu mtendaji wa kampuni hiyo Andre Bothma akisema.

Lesotho ilikuwa nchi ya kwanza ya Afrika kuhalalisha kisheria kilimo cha bangi kwa ajili ya matumizi ya dawa mwaka 2017.

Latest News

“TUTAJIRIDHISHA KABLA YA KUKUBALI CHANJO YA CORONA”- Rais Samia.
14 May 2021 18:24 - Grace Melleor

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amesema kabla ya kupokea chanjo ya virusi vya Corona ni lazi [ ... ]

SOMALIA YATANGAZA KUREJESHA UHUSIANO NA KENYA.
06 May 2021 17:57 - Grace Melleor

Somalia imetangaza kuwa inarejesha mahusiano ya kidiplomasia na nchi jirani ya Kenya baada ya kusitisha mahusiano hayo m [ ... ]

KENYA NA TANZANIA KUONDOA VIKWAZO VYA BIASHARA.
05 May 2021 15:39 - Grace Melleor


Rais Samia Suluhu Hassan amesema Tanzania iko tayari kuwapokea wawekezaji kutoka Kenya pamoja na kuondoa vikwazo visivy  [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2021 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.