Star Tv

Mizinga 41 ya heshima ilipigwa leo Aprili 10 nchini Uingereza, rasi ya Gibraltar na kwenye meli zote za jeshi la nchi hiyo kumkumbuka mume wa Malkia Elizabeth wa Pili, Mwanamfalme Philip aliyeaga dunia jana Ijumaa.

Heshima hiyo ya kijeshi ilitolewa majira ya mchana siku moja tangu ilipotangazwa kuwa Mwanamfalme Phillip amefariki dunia akiwa kwenye kasri wa Windsor baada ya kuugua kwa wiki kadhaa.

Salamu za rambirambi zimeendelea kutolewa kutoka kila pembe ya dunia kukumbuka maisha ya Mwanamfalme Phillip ambaye amekuwa mume na nguzo muhimu katika utawala wa Malkia Elizabeth kwa zaidi ya miaka 70.

Katika salamu zake za pole, kiongozi wa kanisa katoliki duniani Papa Francis amemwelezea mwanamfalme Philip kuwa mtu aliyejitolea kwa ajili ya familia yake na kuwa na mchango mkubwa katika sekta ya elimu.

Mwanamfalme Philip atazikwa kwa heshima zote za kifalme lakini mazishi yake yanapangwa kufanyika kwa taratibu tafauti kutokana na vizuizi vya kupambana na janga la virusi vya corona.

Latest News

“TUTAJIRIDHISHA KABLA YA KUKUBALI CHANJO YA CORONA”- Rais Samia.
14 May 2021 18:24 - Grace Melleor

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amesema kabla ya kupokea chanjo ya virusi vya Corona ni lazi [ ... ]

SOMALIA YATANGAZA KUREJESHA UHUSIANO NA KENYA.
06 May 2021 17:57 - Grace Melleor

Somalia imetangaza kuwa inarejesha mahusiano ya kidiplomasia na nchi jirani ya Kenya baada ya kusitisha mahusiano hayo m [ ... ]

KENYA NA TANZANIA KUONDOA VIKWAZO VYA BIASHARA.
05 May 2021 15:39 - Grace Melleor


Rais Samia Suluhu Hassan amesema Tanzania iko tayari kuwapokea wawekezaji kutoka Kenya pamoja na kuondoa vikwazo visivy  [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2021 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.