Star Tv

Mamlaka za nchini Saudi Arabia zimesema watu waliopata chanjo ya corona peke yake ndio wataruhusiwa kufanya ibada ya Hija mwaka huu huko Mecca.

Wizara ya Hija na Umrah imetoa taarifa kuwa watu waliopata chanjo pekee ndio watakuwa na vigezo vya kujihi mwaka huu 2021 katika mji mtakatifu wa Mecca.

"Watu ambao tayari wamepata chanjo dozi mbili za COVID-19, na wale ambao wamepata chanjo dozi moja ya corona siku 14 kabla ya Hija au mtu ambaye ametoka kupona corona"-Wizara imesema.

Wizara hiyo imesema pia kuwa itazingatia taratibu zote za kujikinga dhidi ya maambukizi ya corona, Ingawa haijawekwa wazi kama sera hiyo itaendelea mpaka wakati wa Hija kuu baadaye mwaka huu.

Saudi Arabia imeripoti kuwa na maambukizi ya virusi vya corona zaidi vya zaidi ya watu 393,000 na zaidi ya vifo 6,700 vinavyotokana na virusi hivyo.

Wizara ya afya ya taifa hilo imesema watu zaidi ya milioni tano wamepata chanjo dhidi ya corona, katika taifa lenye watu zaidi ya milioni 34.

Mwezi uliopita mfalme Salman alimbadilisha Waziri wa Hija, Mwezi mmoja baadaye ilifanyika Hija ndogo katika mfumo mpya wa kihistoria kutokana na changamoto ya virusi vya corona.

Mwaka jana, Waislamu 10,000 ambao ni wakazi wa Saudi Arabia ndio waliruhusiwa katika Hija takatifu mwaka jana, ingawa mara zote huwa ni watu Milioni 2.5 kutoka duniani kote na ndio walishiriki Hija mwaka 2019.

Chanzo: BBCSwahili

Latest News

“TUTAJIRIDHISHA KABLA YA KUKUBALI CHANJO YA CORONA”- Rais Samia.
14 May 2021 18:24 - Grace Melleor

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amesema kabla ya kupokea chanjo ya virusi vya Corona ni lazi [ ... ]

SOMALIA YATANGAZA KUREJESHA UHUSIANO NA KENYA.
06 May 2021 17:57 - Grace Melleor

Somalia imetangaza kuwa inarejesha mahusiano ya kidiplomasia na nchi jirani ya Kenya baada ya kusitisha mahusiano hayo m [ ... ]

KENYA NA TANZANIA KUONDOA VIKWAZO VYA BIASHARA.
05 May 2021 15:39 - Grace Melleor


Rais Samia Suluhu Hassan amesema Tanzania iko tayari kuwapokea wawekezaji kutoka Kenya pamoja na kuondoa vikwazo visivy  [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2021 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.