Star Tv

Marekani imewaamuru baadhi ya wafanyakazi wake na familia zao kuondoka nchini Myanmar kutokana ghasia zinazoendelea.

Katikati ya mwezi uliopita, wizara ya mambo ya nje ya Marekani ilitoa tahadhari kwa wafanyakazi wasio wa dharura kuondoka kwa hiari.

Maandamano ya kila siku kote nchini Myanmar ya kudai kurejeshwa kwa serikali ya kiraia na kuachiwa kwa kiongozi wake Aung San Suu Kyi, yamekabiliwa na ukandamizaji mkubwa kutoka kwa vikosi vya usalama.

Idadi ya watu waliopoteza maisha tangu mapinduzi ya kijeshi inakadiria kufikia watu 520.

Nchi mbalimbali zimeendelea kulaani matumizi ya nguvu yanayotekelezwa jeshi dhidi ya raia.

Marekani, Uingereza na Umoja wa Ulaya zote zimetangaza vikwazo kupinga mapinduzi na ukandamizaji, lakini juhudi hizo za kidiplomasia bado hazijazaa matunda

Latest News

RAIS TSHISEKEDI ADHIBITI BARAZA LAKE JIPYA LA MAWAZIRI.
13 Apr 2021 18:22 - Grace Melleor

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Jumatatu alitangaza baraza jipya la Mawaziri katika hatua ambayo inaimar [ ... ]

MALIPO YA NDEGE MPYA TATU YAKAMILIKA.
13 Apr 2021 18:04 - Grace Melleor


Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema tayari serikali imekamilisha malipo ya ununuzi wa ndege mpya tatu.

WASAFIRI KUTOKA KENYA KUINGIA KARANTINI KWANZA IRELAND.
12 Apr 2021 13:43 - Grace Melleor

Wasafiri wanaoelekea Ireland kutoka Kenya watalazimika kujitenga kwa wiki mbili baada ya kuwasili katika nchi hiyo ya ba [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2021 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.