Watu nane wakiwemo wanawake wenye asili ya bara Asia wameuawa katika ufyatuaji risasi jimboni Georgia nchini Marekani.
Jeshi la Polisi limethibitisha kutokea kwa mauaji hayo wakati Korea Kusini ikidai waathirika wanne kati yao walikuwa na asili ya Korea.
Mwanaume mwenye umri wa miaka 21 anashikiliwa kwa tuhuma za kuhusika na mashambulizi yote.
Aidha bado sababu za kutekelezwa kwa shambulizi hilo hazijabainika.
Hata hivyo,uhalifu wa chuki dhidi ya Wamarekani wenye asili ya Asia umeongezeka zaidi katika miezi ya hivi karibuni ukichochewa na shutuma za kusambaza virusi vya Covid-19.
Katika hotuba yake wiki iliyopita, Rais Joe Biden alilaani uhalifu mbaya wa chuki dhidi ya Wamarekani wenye asili ya Asia ambao wameshambuliwa, kunyanyaswa, kulaumiwa na kupuuzwa.
ChanzoBBCSwahili