Vifo vya waandamanaji wawili wanaopinga mapinduzi nchini Myanmar, leo hii vimezusha lawama mpya kutoka Umoja wa Mataifa dhidi ya utawala wa kijeshi.
Tamko la umoja huo linatolewa wakati waombolezaji wanajiandaa na mazishi ya binti, ambaye amekuwa alama ya kuupinga utawala wa kijeshi.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres amelaani matumizi makubwa ya nguvu katika makabiliano yaliyotokea jana Jumamosi ambayo wahudumu wa kitengo cha dharura wanasema mtu mmoja amekufa na wengine kadhaa wamejeruhiwa.
Katika siku za karibuni, mamlaka za Myanmar zimeongeza mbinu kuyakabili maandamano ya umma yanayoshinikiza kurudishwa madarakani kwa kiongozi wa kiraia aliyeondolewa madarakani Aung San Suu Kyi.