Star Tv

Baraza la seneti nchini Marekani limemuondolea mashitaka rais wa zamani wa nchi hiyo Donald Trump, ya kuchochea shambulio baya dhidi ya jengo la bunge.

Hii ni kufuatia vurugu zilizosababishwa na kushindwa kwake katika uchaguzi, Ambapo maseneta 57 walipiga kura ya kumtia hatiani rais huyo wa zamani huku 43 wakikataa mashtaka dhidi yake.

Warepublican saba waliungana na Wademocrat wote kumtia hatiani Trump, lakini idadi hiyo ilikuwa chini sana ya kihunzi cha theluthi mbili iliyohitajika.

Matokeo hayo yameacha migawiko isiyo na utatuzi nchini humo kuhusiana na siasa za Trump zilizosababisha shambulio baya zaidi la ndani dhidi ya mmoja ya mihimili mitatu ya demokrasia ya Marekani.

Ingawa aliondolewa hatia kuhusu shitaka pekee la kuchochea uasi, kesi hii ilishuhudia idadi kubwa zaidi ya maseneta kuwahi kupiga kura kumtia hatiani rais wa chama chao kwa makosa makubwa na madogo.

Latest News

RAIS MAGUFULI AWAONYA WAKANDARASI WANAOCHELEWESHA MIRADI.
24 Feb 2021 13:33 - Grace Melleor

Rais John Magufuli amezindua barabara ya juu eneo la Ubungo ambayo imepewa jina la Marehemu John Kijazi, ambaye alikuwa  [ ... ]

MWILI WA BALOZI WA ITALIA WASAFIRISHWA KWENDA ROMA.
24 Feb 2021 09:52 - Grace Melleor

Mwili wa balozi wa Italia aliyeuawa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo katika jaribio la utekaji nyara uliotibuka s [ ... ]

MWANASIASA WA UPINZANI WA RWANDA AUAWA.
22 Feb 2021 07:59 - Grace Melleor

Mwanasiasa wa upinzani na raia wa Rwanda anayeishi mafichoni nchini Afrika Kusini ameuawa kwa kupigwa risasi.

Other Articles

Social Media

Copyright © 2021 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.