Star Tv

Wajumbe wa nchi wanachama wa Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC) wanatarajia kukutana mjini New York baadaye leo kumchagua mwendesha mashitaka mpya wa mahakama hiyo.

Wagombea tisa ikiwa ni pamoja na majaji wawili mmoja kutoka Nigeria na mmoja kutoka Uganda, wako katika orodha ya kumrithi Mgambia Bi Fatou Bensouda, ambaye muhula wake kama Mwendesha mashitakaMkuu wa mahakama hiyo unamalizika mwezi Juni mwaka huu.

Bi Bensouda amekuwa Mwendesha mashitaka Mkuu wa ICC tangu mwaka 2011- baada ya kuchukua nafasi ya wakili Muargentina Luis Moreno Ocampo.

Katika muhula wake madarakani, aliweza kuwatia hatiani washitakiwa Zaidi kuliko mtangulizi wake- na hivi karibuni ikiwa akiwa ni muasi wa zamani wa Uganda kamandaDominic Ongwen ambaye mwezi huu alipatikana na hatia za uhalifu wa kivita.

Hatahivyo, Mwanamama huyo alikabiliwa na ukosoaji mkubwa hususani kuhusu kesi zake kuwalenga Waafrika.

Mwezi Juni mwaka jana, Bensouda alizuiwa kusafiri nchini Marekani wakati rais wa Marekani wa wakati huo Donald Trump aliposaini sheria ya rais inayoweka vikwazo vya fedha dhidi yake.

Watu wengine wanaowania nafasi ya Bensouda ni pamoja na:

1. Karim Khan - Wakili Kutoka Uingereza

2. Robert Petit - Mwendesha mashitaka kutoka Canada

3. Susan Okalany - Jaji kutoka Uganda

4. Morris Anyah - Jaji kutoka Nigeria

5. Fergal Gaynor - Mwendesha mashitaka kutoka IRELAND

6. Fernandez Castresana - Mwendesha mashitaka kutoka Uhispania

7. Francesco Lo Voi- Mwendesha mashitaka kutoka Italia.

8. Brigitte Raynaud – Mwendesha mashitaka kutoka Ufaransa

9. Richard Roy – Wakili kutoka Canada

Nchi wanachama wa ICC zilishindwa kufikia maelewano kuhusu nafasi hiyo licha ya kujaribu wiki za hivi karibuni na sasa watapiga kura huko New-York katika Umoja wa Mataifa.

Muda wa Mwendesha mashataka mkuu Fatou Bensouda raia wa Gambia utamalizika mwezi Juni na atakayeingia ataendelea na kesi ngumu ikiwemo uhalifu wa kivita Afghanistan, na uchunguzi kuhusu vita kati ya Israel na Gaza vya 2014.

 

Latest News

RAIS MAGUFULI AWAONYA WAKANDARASI WANAOCHELEWESHA MIRADI.
24 Feb 2021 13:33 - Grace Melleor

Rais John Magufuli amezindua barabara ya juu eneo la Ubungo ambayo imepewa jina la Marehemu John Kijazi, ambaye alikuwa  [ ... ]

MWILI WA BALOZI WA ITALIA WASAFIRISHWA KWENDA ROMA.
24 Feb 2021 09:52 - Grace Melleor

Mwili wa balozi wa Italia aliyeuawa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo katika jaribio la utekaji nyara uliotibuka s [ ... ]

MWANASIASA WA UPINZANI WA RWANDA AUAWA.
22 Feb 2021 07:59 - Grace Melleor

Mwanasiasa wa upinzani na raia wa Rwanda anayeishi mafichoni nchini Afrika Kusini ameuawa kwa kupigwa risasi.

Other Articles

Social Media

Copyright © 2021 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.