Star Tv

Rais wa Marekani Joe Biden amemuonya kiongozi wa Urusi Vladimir Putin kuhusu kuingilia uchaguzi wa nchi hiyo.

Ikulu ya White House imeeleza kuwa Biden amemuonya Rais putin kupitia mawasiliano yao ya kwanza waliyofanya kwa njia ya simu.

Mazungumzo hayo ni pamoja na majadiliano kuhusu maandamano ya upinzani yanayoendelea nchini Urusi na kuongezwa kwa mkataba wa silaha za nyuklia wa Marekani na Urusi

Bwana Putin alimpongeza rais mpya wa Marekani kwa kushinda uchaguzi,kwa mujibu wa taarifa ya Urusi.

Pande zote mbili zilisema zilikubaliana kudumisha mahusiano kwa maslahi mapana ya nchi zao.

Rais Biden aliweka wazi kuwa, "Marekani itasimama kidete kutetea maslahi ya taifa lake kwa vitendo vya Urusi vinavyotuathiri sisi au washirikawetu''- ilisema taarifa ya Marekani.

Ikulu ya Marekani imesema marais hao waliozungumza kwa simu siku ya Jumanne pia walijadili kuhusu mashambulizi ya mtandaoni ya kampuni ya SolarWinds, ambayo Moscow ilinyooshewa kidole, huku ripoti zikieleza kuwa Kremlin iliwafadhili wanajeshi wa Marekani nchini Afghanistan, na sumu ya mwanaharakati wa upinzani wa Urusi Alexei Navalny.

Maafisa wa urusi wamesema Bw. Putin ''ameona kuwa kuweka sawa mahusiano kati ya Urusi na Marekani kutafanya kufikiwa kwa malengo na kulinda maslahi ya nchi zote mbili-ukizingatia jukumu walilonalo la kulinda usalama na uimara duniani.

"Kwa ujumla, mazungumzo kati ya viongozi wa Urusi na Marekani yalikuwa ya biashara na ya asili ya kweli"- taarifa ya Kremlin iliongeza.

Viongozi hao wawili walionekana kutia saini makubaliano ya kurejesha New Start, makubaliano ya wakati wa Obama ambayo yanapunguza viwango vya silaha, makombora na virusha makombora miongoni mwa silaha za nyuklia za Marekani na Urusi.

Chanzo na BBC

Latest News

RAIS MAGUFULI AWAONYA WAKANDARASI WANAOCHELEWESHA MIRADI.
24 Feb 2021 13:33 - Grace Melleor

Rais John Magufuli amezindua barabara ya juu eneo la Ubungo ambayo imepewa jina la Marehemu John Kijazi, ambaye alikuwa  [ ... ]

MWILI WA BALOZI WA ITALIA WASAFIRISHWA KWENDA ROMA.
24 Feb 2021 09:52 - Grace Melleor

Mwili wa balozi wa Italia aliyeuawa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo katika jaribio la utekaji nyara uliotibuka s [ ... ]

MWANASIASA WA UPINZANI WA RWANDA AUAWA.
22 Feb 2021 07:59 - Grace Melleor

Mwanasiasa wa upinzani na raia wa Rwanda anayeishi mafichoni nchini Afrika Kusini ameuawa kwa kupigwa risasi.

Other Articles

Social Media

Copyright © 2021 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.