Star Tv


Rais mteule wa Marekani Joe Biden amepokea chanjo ya Pfizer, kuzuia maambukizi ya virusi vya Corona vinavyosababisha ugonjwa hatari wa COVID-19.

Biden amepewa chanjo hiyo na kuonekana moja kwa moja na Wamarekani na anakuwa kiongozi mwingine wa juu baada ya Makamu wa rais Mike Pence na Spika wa Bunge Nancy Pelosi pia kupata chanjo hiyo.

Rais huyo mteule ameeleza sababu ya kupata chanjo hiyo hadharani: “Niko tayari," Joe Biden alisema, akiinua mkono wake.

Rais mteule aliongozana na mkewe, ambaye pia alipokea chanjo hiyo, Na baadaye Joe Biden alizungumza kwa muda mrefu na daktari aliyemdunga chanjo hiyo kumshukuru kwa kazi yote iliyofanywa na wafanyakazi wa afya.

"Ninyi ni mashujaa na tunawaenzi sana," alisema kabla ya kuwaambia waandishi wa habari: "Ninafanya hivi kuonyesha kuwa watu wanapaswa kuwa tayari kupata chanjo wakati itakapopatikana, wasiwi na hofu yoyote. "


Wakati Marekani inakabiliwa na mlipuko wa pili ambao unaendelea kusababisha vifo vingi, Joe Biden alitoa wito kwa Wamarekani kuheshimu hatua za usafi, na kuepuka kusafiri wakati wa sikukuu za Krismasi na mwaka mpya.

Biden amekuwa akisema baada ya kuingia madarakani, serikali yake itatoa chanjo Milioni 100 kwa siku 100 za Kwanza madarakani.

 

Latest News

WANAOGESHA MAGARI BARABARANI HOVYO KUWAJIBISHWA BILA HURUMA.
20 Jan 2021 14:26 - Grace Melleor

Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Mhandisi Godfrey Kasekenya, ameitaka Bodi ya mfuko wa Barabara (RfB) kutumia vifungu [ ... ]

KENYA KUPOKEA DOZI MILIONI 24 ZA CHANJO YA CORONA.
20 Jan 2021 14:06 - Grace Melleor

Kenya inatarajia kupokea dozi milioni 24 za chanjo ya ugonjwa corona iliyotengenezwa na kapuni ya Astrazeneca na chuo ki [ ... ]

BIDEN AJIANDAA KUINGIA IKULU, HUKU TRUMP AKISUSIA KUHUDHURIA KUAPISHWA KWAKE.
20 Jan 2021 08:14 - Grace Melleor

Rais mteule wa Marekani Joe Biden aliwasili Washington katika mkesha wa sherehe ya kuapishwa kwake, wakati mtangulizi wa [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2021 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.