Star Tv

Virusi vya Corona katika bara la Ulaya vimeendelea kuwa tishio hasa kwa viongozi wakuu wa mataifa hayo, ambapo taarifa kutoka ofisi ya Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron imeleeza kuwa Rais huyo amekutwa na virusi hivyo.

Rais Macron ambaye ni mwenye miaka 42 alifanya vipimo mara tu alipoanza kujisikia dalili, na sasa anajitenga kwa muda wa siku saba, taarifa kutoka Ikulu zimeeleza.

Na kuongeza kusema, Bwana Macron bado anaendelea na shughuli za kuiongoza nchi huku akiwa amejitenga.

Wiki hii, Ufaransa iliweka marufuku ya watu kutotembea muda wa usiku baada ya maambukizi ya corona kuongezeka.

Ufaransa imethibitisha maambukizi Milioni mbili tangu janga la corona lilivyoibuka, huku kukiwa na vifo 59,400 kwa mujibu wa data kutoka chuo kikuu cha Johns Hopkins.

Haijajulikana ni vipi bwana Macron alipata maambukizi hayo na watu waliokutana naye wameainishwa, Ambapo Waziri Mkuu Jean Castex, 55, pia amejitenga kwasababu walikutana na Rais kwa karibu.

Taarifa kutoka ofisi ya rais haijasema kama mke wa Rais huyo Bi. Brigitte, ambaye ana miaka 67, kama alikutwa na virusi vya corona pia.

Bwana Macron ni miongoni mwa viongozi wakubwa duniani waliopata ugonjwa huo.

Rais wa Marekani Donald Trump alipata corona mwezi Oktoba na kumfanya alazwe siku tatu hospitalini.

Waziri mkuu wa Uingereza Boris Johnson pia alipata virusi vya corona na kulazwa mpaka chumba cha wagonjwa mahututi mwezi Machi.

Mapema wiki hii, wakati Ufaransa imeweka marufuku dhidi ya corona kwa awamu ya pili baada ya maambukizi kuongezeka, Na siku ya Jumatano Ufaransa imethibitisha zaidi ya maambukizi mapya 17,700.

Latest News

Mgogoro wa Maji unatishia Amani Duniani, inasema ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa...
21 Mar 2024 14:18 - Kisali Shombe

Siku ya Maji Duniani ambayo inafanyika tarehe 22 Machi ikiwa na kaulimbiu: 'Maji kwa Ustawi na Amani. Ambapo maji ni moj [ ... ]

Matarajio katika mkutano wa BRICS nchini Afrika Kusini, Jumanne tarehe 22/2023
21 Aug 2023 12:14 - Kisali Shombe

Mkutano huo ambao utafanyikia Johannesburg nchini Afrika Kusini siku ya Jumanne, tarehe 22 Agosti 2023, unatarajiwa kuhu [ ... ]

Rais Ramaphosa Kuwa Mwenyeji wa Rais Xi Jinping wa China
21 Aug 2023 11:11 - Kisali Shombe

Rais Cyril Ramaphosa Jumanne ya tarehe 22 Agosti 2023, atakuwa mwenyeji wa Mheshimiwa Rais Xi Jinping wa China katika Zi [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2024 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.