Star Tv

Rais Mteule nchini Marekani kupitia Chama cha Demokrats amemteua Anthony Blinken kuwa Waziri wa mambo ya nje.

Duru za kisiasa nchini Marekani zimeripoti kuwa rais huyo mteule wa Marekani Joe Biden amemteua Anthony Blinken kuwa Waziri wa mambo ya nje, atakapochukua kiti cha urais rasmi.

Bw. Blinken ana uhusiano wa karibu na Bw Biden kwa takribani miaka 20, ambaye anaelezwa kuwa na uzoefu wa masuala ya kigeni.

Anafahamika kama mtu anayeunga mkono ushirika dhabiti na mataifa mengi, akisema mapema mwaka huu kwamba matatizo kama vile mabadiliko ya hali ya hewa, janga la corona na utengenezaji wa silaha hatari hayawezi kutatuliwa na Marekani peke yake.

Wakati mmoja aliwahi kuwa Naibu waziri wa mambo ya nje chini ya utawala wa rais wa zamani Barack Obama ambapo alisaidia kuboresha masuala ya ushirikiano na mataifa yaMashariki ya kati.

Bw Bilken, mwenye umri wa miaka 58, alisomea Ufaransa, na baadaye katika Chuo Kikuu cha Harvard University na Cho Kikuu cha Sheria cha Colombia.

Latest News

BIDEN KUSAINI MAAGIZO 12 YA RAIS.
17 Jan 2021 07:08 - Grace Melleor

Rais mteule wa Marekani Joe Biden atatia saini maagizo 12 ya rais siku ya kuapishwa kwake kuwa rais wiki ijayo ili kushu [ ... ]

MUSEVENI AWAONYA WAFUASI WA UPINZANI KUTOZUA GHASIA.
17 Jan 2021 06:10 - Grace Melleor

Rais wa muda mrefu nchini Uganda Yoweri Museveni jana Jumamosi ameonya kuwa vikosi vya usalama vitatumia nguvu kuzima ju [ ... ]

WATU WAWILI WANUSURIKA KUAWA NA WANANCHI WENYE HASIRA KALI.
17 Jan 2021 05:42 - Grace Melleor

Watu wawili wakazi wa Manispaa ya Musoma mkoani Mara wamenusurika kuawa na wananchi wenye hasira kali kutoka kwa vijana  [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2021 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.