Star Tv

Mahasimu wakubwa kwenye uchaguzi mkuu wa mwezi Novemba nchini Marekani Rais Donald Trump wa Republican na Joe Biden wa Democratic, wametumia mdahalo wao wa kwanza kushambuliana jinsi familia zao zilivyofaidika na kuwapo kwao madarakani.

Mdahalo kati ya wagombea wawili katika uchaguzi wa urais wa Marekani umefanyika katika hali ya mvutano na matusi, huku kila mmoja akimshtumu mwenzake.

Wawili hawa walitofautiana takribani kwenye kila swali walilorushiwa na mwenyekiti wa mdahalo huo: kuanzia masuala ya afya, usalama, hadi ya kifamilia.

Wakati Biden alipokuwa akizungumzia jinsi mikataba ya kibiashara ya Marekani na China isivyoleta tija iliyokusudiwa, Trump alimkatiza akitaja kuhusika kwa mtoto wa Biden aitwaye Hunter Biden kwenye biashara nje ya nchi, hasa Ukraine.

Kwa upande wake, Biden alisema ingechukua usiku mzima kuzungumzia familia ya Trump, laiti angelitaka hilo.

Mdahalo huo ulifuatiliwa na mamilioni ya watu, hasa Wamarekani ambao wengi walitarajia kuwa wagombea hao wawili watazungumzia masuali nyeti yanayotakiwa kupewa kipaumbelea katika nchi hiyo inayoendelea kuzongwa na ugonjwa hatari wa COVID-19 unaosababishwa na virusi vya Corona.

Mdahalo huo umefanywa kwa msururu wa kurushiana vijembe , ambavyo ni pamoja na Trump kuhoji ujasusi wa Biden na Biden akimwita Trump kichekesho, akimnyamazisha, kwa hasira, "Je! Utanyamaza, jamani?"

Mdahalo huo uliendeshwa na Chris Wallace, mwandishi wa kituo cha televisheni cha Fox News.

Mdahalo huo uligubikwa na masuala kuhusu janga la COVID-19, Mahakama Kuu, uchumi, ubaguzi wa rangi na machafuko yaliyokumba baadhi ya mijini, sera za kila mmoja wa wagombea na 'ukweli wa matokeo ya uchaguzi'.

Swali la kwanza lilihusiana na uteuzi wa Jaji mpya wa Mahakama Kuu, Amy Coney Barrett, siku chache zilizopita.

Mbali ya mikataba ya kibiashara, mdahalo huo uliofanyika usiku wa kuamkia leo Septemba 30,2020 ulitandwa pia na shutuma na tuhuma baina yao kuhusiana na masuala kadhaa, kuanzia janga la virusi vya corona, mfumo wa afya, uchumi, usalama na ubaguzi wa rangi, hadi athari za mabadiliko ya tabia nchi, ambapo Biden aliahidi kuirejesha Marekani kwenye Mkataba wa Paris ambao unalenga kupunguza uzalishaji wa gesi chafu.

Latest News

ETHIOPIA YASEMA HAITISHWI NA TAMKO LA RAIS DONALD TRUMP.
24 Oct 2020 16:54 - Grace Melleor

Waziri mkuu wa Ethiopia amesema nchi yake "haitakubali vitisho vya aina yoyote" baada ya Rais Donald Trump kusema kuwa M [ ... ]

RAIS TSHISEKEDI ATANGAZA MASHAURIANO YA UMOJA KWA MUUNGANO TAWALA.
24 Oct 2020 06:41 - Grace Melleor

Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Felix Tshisekedi, katika hotuba yake kwa taifa aliyoitoa siku ya Ijumaa wiki hi [ ... ]

SEKTA YA AFYA NCHINI YAPATA NEEMA KUTOKA USWISI.
23 Oct 2020 15:23 - Grace Melleor

Serikali imepokea msaada wa Faranga za Uswisi Milioni 15.75 sawa na shilingi Bilioni 39.59 kwa ajili ya kugharamia mradi [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2020 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.