Star Tv

Serikali ya Libya yadai kuuteka mji muhimu kutoka kwa hasimu wake Khalifa Haftar.

Vikosi vilivyo na mafungamano na serikali ya Libya inayotambulika kimataifa vimesema vimechukua udhibiti wa mji muhimu kutoka kwa mahasimu wao hii leo.

Haya yanatokea siku moja tu baada ya vikosi hivyo kuchukua udhibiti wa mji mkuu Tripoli.

Katika wiki za hivi majuzi vikosi hivyo vimepiga hatua kubwa katika kuyanyakua maeneo yaliyokuwa yanadhibitiwa na mbabe wa kivita Khalifa Haftar.

Msemaji wa serikali ya Waziri Mkuu Fayez el-Sarraj, Mohammed Gnounou amesema leo kuwa vikosi vya serikali vimeudhibiti kikamilifu mji wa Tarhouna, ulioko kilomita 90 kusini mashariki mwa Tripoli.

Msemaji wa jeshi la serikali hiyo inayotambulika kimataifa amesema vikosi vya serikali vimeingia katika mji wa Tarhouna bila mapigano baada ya vikosi vya Haftar kuondoka katika mji huo na kuelekea jangwani.

Latest News

RAIS MAGUFULI AWAONYA WAKANDARASI WANAOCHELEWESHA MIRADI.
24 Feb 2021 13:33 - Grace Melleor

Rais John Magufuli amezindua barabara ya juu eneo la Ubungo ambayo imepewa jina la Marehemu John Kijazi, ambaye alikuwa  [ ... ]

MWILI WA BALOZI WA ITALIA WASAFIRISHWA KWENDA ROMA.
24 Feb 2021 09:52 - Grace Melleor

Mwili wa balozi wa Italia aliyeuawa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo katika jaribio la utekaji nyara uliotibuka s [ ... ]

MWANASIASA WA UPINZANI WA RWANDA AUAWA.
22 Feb 2021 07:59 - Grace Melleor

Mwanasiasa wa upinzani na raia wa Rwanda anayeishi mafichoni nchini Afrika Kusini ameuawa kwa kupigwa risasi.

Other Articles

Social Media

Copyright © 2021 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.