Star Tv

Watu kadhaa wamepoteza Maisha katika machafuko yaliyoibuka wakati wa kura ya maoni ya Katiba na uchaguzi wa wabunge yaliyofanyika Jumapili Machi 22,2020 huku wengine wakijeruhiwa nchini Guinea.

Kwa upande wa vyama vya upinzani wanaelezwa kususia zoezi hilo ambalo pia lilipingwa na Jumuiya ya kimataifa kwa kudhania kuwa uchaguzi huo unakusudia kuzuia muhula wa tatu wa rais Alpha Condé  kutaka kuwania tena uongozi wa nchi hiyo.

Hata hivyo wizara ya usalama imebaini kwamba watu wanne ndio waliuawa kwa siku ya jana ikiwa ni pamoja na wawili katika ghasia, mmoja kufuatia ajali na mwengine kufuatia mshtuko wa moyo, bila maelezo zaidi.

Taarifa hiyo ya wizara ya usalama imeongeza kuwa maafisa 9 kutoka kitengo maalum cha usalama wa uchaguzi, pamoja na maafisa 7 wa polisi, walijeruhiwa vibaya, wakati vuguvugu linalodai kulinda katiba ya nchi (FNDC) limetangaza kwamba wafuasi wake kadhaa wamejeruhiwa kwa risasi.

Kwa mujibu wa Wizara ya Usalama nchini humo imesema kuwa waandamanaji walishambulia vituo vya kupigia kura, wakiharibu vifaa vya kupigia kura pamoja na kuchoma vifaa vya uchaguzi katika miji kadhaa nchini humo na katika maeneo ya mji wa Conakry yenye wafuasi wengi wa upinzani, kwa mlujibu wa Wizara ya Usalama.

Watu kadhaa tayari wamekamatwa kwa makosa ya kuhusika katika machafuko na kuatarisha usalama wa raia, kumiliki na kutumia silaha za moto kinyume cha sheria, uharibifu wa mali ya umma, kuchoma moto vifaa vya uchaguzi, kupiga na kufanya uasi dhidi ya serikali, wizara ya usalama imeongeza.

                                  Mwisho.

Latest News

Mgogoro wa Maji unatishia Amani Duniani, inasema ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa...
21 Mar 2024 14:18 - Kisali Shombe

Siku ya Maji Duniani ambayo inafanyika tarehe 22 Machi ikiwa na kaulimbiu: 'Maji kwa Ustawi na Amani. Ambapo maji ni moj [ ... ]

Matarajio katika mkutano wa BRICS nchini Afrika Kusini, Jumanne tarehe 22/2023
21 Aug 2023 12:14 - Kisali Shombe

Mkutano huo ambao utafanyikia Johannesburg nchini Afrika Kusini siku ya Jumanne, tarehe 22 Agosti 2023, unatarajiwa kuhu [ ... ]

Rais Ramaphosa Kuwa Mwenyeji wa Rais Xi Jinping wa China
21 Aug 2023 11:11 - Kisali Shombe

Rais Cyril Ramaphosa Jumanne ya tarehe 22 Agosti 2023, atakuwa mwenyeji wa Mheshimiwa Rais Xi Jinping wa China katika Zi [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2024 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.