Star Tv

Kirusi cha corona chazidi kusambaa duniani kwa kutia mguu Magharibi mwa Afrika ambapo mtu wa kwanza aliye na kirusi cha corona katika eneo la chini ya jangwa la Sahara Magharibi mwa Afrika amegunduliwa nchini Nigeria.

Waziri wa Afya wa Nigeria Osagie Ehanire ameeleza katika taarifa aliyotoa kupitia ukurasa wake wa kijamii wa Twitter mapema leo kwamba, mtu huyo ni raia wa Italia anayefanya kazi nchini humo, ambaye alirejea Nigeria mapema wiki hii akitokea mjini Milan, Italia.

Amesema hali ya mtu huyo si mbaya na tayari amelazwa katika hospitali ya magonjwa ya kuambukiza ya Yaba mjini Lagos.

Kabla ya Nigeria, kulikuwa kumeripotiwa kesi mbili tu za maambukizi ya kirusi cha corona barani Afrika, moja ikiwa ni katika ya nchi ya Misri na nyingine nchini Algeria.

Wakati huohuo Lithuania nayo pia imemgundua mtu mwenye kirusi cha corona nchini humo.

Maafisa wa afya wa Ireland ya Kaskazini nao pia wametangaza kugunduliwa mtu aliyekumbwa na kirusi cha corona katika eneo hilo na kuifanya idadi ya watu walioambukizwa kirusi hicho nchini Uingereza kufikia 16.

Mbali na China, ambayo ni kitovu cha maambukizi ya kirusi cha corona, nchi za Ulaya Magharibi zina idadi kubwa zaidi ya watu waliokumbwa na kirusi hicho.

Baada ya watu waliofariki kwa kirusi cha corona nchini Italia kuongezeka na kufikia 17, Ufaransa imetangaza kuwa idadi ya watu waliokumbwa na kirusi hicho nchini humo imefikia 40 wakati idadi hiyo nchini Ujerumani ni 38.

                                             Mwisho.

Latest News

TEMBO 170 KUPIGWA MNADA NAMIBIA.
03 Dec 2020 10:05 - Grace Melleor

Tembo 170 watapigwa mnada nchini Namibia kwa kile kilichobainishwa kuwa ni adha ya kuongezeka kwa ukame huku kukishuhudi [ ... ]

BOKO HARAM WAKIRI KUTEKELEZA MAUAJI YA WAKULIMA 78.
02 Dec 2020 08:42 - Grace Melleor

Wanamgambo wa kundi la Kiislamu la Boko Haram wametoa video mpya ambayo inasema wapiganaji wake wa Boko Haram ndio walio [ ... ]

BOBI WINE AAHIRISHA KAMPENI ZA URAIS.
02 Dec 2020 08:19 - Grace Melleor

Mgombea wa urais nchini Uganda Robert Kyagulanyi, anayefahamika zaidi kama Bobi Wine ameahirisha kampeni zake.

Other Articles

Social Media

Copyright © 2020 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.