Star Tv

Serikali ya umoja wa kitaifa nchini Libya (GNA) yenye makao yake makuu Tripoli, inayotambuliwa na Umoja wa Mataifa, imetangaza usiku wa tarehe 18 kuamkia 19 Februari kwamba imesitisha ushiriki wake katika mazungumzo yaliyokuwa yakiendelea huko Geneva.

GNA imesema imechukuwa uamuzi huo kutokana na ukiukwaji wa mara kwa mara wa makubaliano ya kusitisha mapigano yaliyofikiwa tangu mwezi Januari.

Serikali ya umoja wa kitaifa ya Waziri Mkuu Fayez el-Sarraj imebaini katika taarifa kwamba inajiondoa katika mazungumzo hayo ya amani huko Geneva hadi pale hatua itakapopitishwa dhidi ya  kiongozi Khalifa Haftar ambaye wamemuita mvamizi, ambapo askari wake wamekuwa wakijaribu kuchukua udhibiti wa Tripoli tangu mwezi Aprili mwaka jana.

GNA imevishutumu vikosi vya waasi kwa kukiuka mara kwa mara makubaliano ya kiusitisha mapigano yaliyofikiwa tangu mwezi uliopita. Makabiliano ya mwisho yalitokea Februari 18 alaasiri wakati makombora karibu kumi na tano yalipoanguka kwenye bandari za Tripoli na Al-Chaab.

Raia watatu waliuawa na wengine watano kujeruhiwa, kwa mujibu wa msemaji wa wizara ya afya ya Libya, Amine al-Hachemi.

Mazungumzo ya amani yaliyokuwa yakifanyika huko Geneva, Uswisi, kwa sasa, yamesitishwa.

                                                                         Mwisho. 

 

Latest News

TEMBO 170 KUPIGWA MNADA NAMIBIA.
03 Dec 2020 10:05 - Grace Melleor

Tembo 170 watapigwa mnada nchini Namibia kwa kile kilichobainishwa kuwa ni adha ya kuongezeka kwa ukame huku kukishuhudi [ ... ]

BOKO HARAM WAKIRI KUTEKELEZA MAUAJI YA WAKULIMA 78.
02 Dec 2020 08:42 - Grace Melleor

Wanamgambo wa kundi la Kiislamu la Boko Haram wametoa video mpya ambayo inasema wapiganaji wake wa Boko Haram ndio walio [ ... ]

BOBI WINE AAHIRISHA KAMPENI ZA URAIS.
02 Dec 2020 08:19 - Grace Melleor

Mgombea wa urais nchini Uganda Robert Kyagulanyi, anayefahamika zaidi kama Bobi Wine ameahirisha kampeni zake.

Other Articles

Social Media

Copyright © 2020 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.