Star Tv

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amewasili katika Jiji la Harare nchini Zimbabwe ambapo anafanya Ziara Rasmi ya Kitaifa ya siku 2 kwa mwaliko wa Rais wa Zimbabwe, Mhe. Emmerson Mnangagwa.

Katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Robert Mugabe, Mhe. Rais Magufuli amepokelewa rasmi na mwenyeji wake, Mhe. Rais Mnangagwa kisha kukagua gwaride rasmi lililoandaliwa kwa ajili yake na kupigiwa mizinga 21.

Baadaye  Mhe. Rais Magufuli amekuwa na mazungumzo ya falagha na mwenyeji wake, Mhe. Rais Munangagwa na kisha kuhudhuria Dhifa ya Kitaifa iliyoandaliwa na Mhe. Rais Mnangagwa kwa heshima yake.

Leo,Mhe. Rais Magufuli atafanya mazungumzo rasmi na mwenyeji wake na kisha atatembelea na kuweka shada la maua katika eneo la mashujaa wa ukombozi wa Zimbabwe.

Katika ziara hii Mhe. Rais Magufuli ameongozana na viongozi mbalimbali wakiwemo Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara Ndg. Philip Mangula, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi, Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Luhaga Mpina na Waziri wa Kilimo Mhe. Japhet Hasunga.

 

 

 

Latest News

Mgogoro wa Maji unatishia Amani Duniani, inasema ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa...
21 Mar 2024 14:18 - Kisali Shombe

Siku ya Maji Duniani ambayo inafanyika tarehe 22 Machi ikiwa na kaulimbiu: 'Maji kwa Ustawi na Amani. Ambapo maji ni moj [ ... ]

Matarajio katika mkutano wa BRICS nchini Afrika Kusini, Jumanne tarehe 22/2023
21 Aug 2023 12:14 - Kisali Shombe

Mkutano huo ambao utafanyikia Johannesburg nchini Afrika Kusini siku ya Jumanne, tarehe 22 Agosti 2023, unatarajiwa kuhu [ ... ]

Rais Ramaphosa Kuwa Mwenyeji wa Rais Xi Jinping wa China
21 Aug 2023 11:11 - Kisali Shombe

Rais Cyril Ramaphosa Jumanne ya tarehe 22 Agosti 2023, atakuwa mwenyeji wa Mheshimiwa Rais Xi Jinping wa China katika Zi [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2024 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.